Mwanza, 9 Oktoba 2018: Washindi wa michuano ya Rock City Marathon 2018 wanatarajiwa kuondoka na zawadi zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 30 pamoja na medali, imefahamika. Mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Akizungumza jijini Mwanza leo, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo zinazoratibiwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI), Bw. Zenno Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.

Kwa upande wa mbio za Kilomita 21, Ngowi alisema, pamoja na medali washindi wa kwanza kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 3/- kila mmoja, sh. Mil 1/- kwa washindi wa pili na sh. 750,000/- kwa washindi wa tatu huku washindi wanne hadi wa kumi wakiibuka na zawadi za pesa taslimu na medali kila mmoja.

“Mbio za kilomita tano tunatarajia kwamba zitaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza sambamba na baadhi ya wakuu wa mikoa kanda ya Ziwa ambao pia watajumuika na baadhi ya viongozi waandamizi wa mikoa hiyo wakiwemo wabunge, viongozi na wafanyakazi wa mashirika na makampuni mbalimbali yaani corporates pamoja na ndugu zetu wenye ualbino,’’alisema.

Wadhamini watakaoshiriki katika mbio hizo ni pamoja na kampuni za Puma Energy Tanzania, Tiper, TANAPA, TTB, Nssf, Gold Crest, New Mwanza Hotel, Cf Hospital, CocaCola, Metro Fm, Ef Outdoor, Kk Security, Belmont Fairmount Hotel , Bigie Customs na Global Education Link.

Alibainisha kuwa mbio za Km 5 zitahusisha watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino ambapo washindi kwa upande wa mashirika watapatiwa zawadi za utambuzi ikiwemo medali na vyeti vya ushiriki huku pesa zikielekezwa kwa washiriki wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino.
Baadhi ya Washiriki waliowahi kushiriki mashindano hayo ya Rock City Marathon.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...