Mgeni Rasmi katika wiki maadhimisho ya Usalama na Afya Barabarani ACP Abdi Isango Kamishna msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Oparesheni Kitengo cha Usalama Barabarani Taifa, anamuwakilisha kamanda wa kikosi cha usalama wa barabarani Taifa akizindua rasmi shughuli hizo za upimaji wa afya kwa madereva wasafirishao mizigo masafa ya mbali iliyoandaliwa na North Star alliance kwa kushirikiana na Puma Energy Foundation , Impala Terminals na Trafigura Foundation.
Ndg. Henry Mgala Bantu mtaalam wa usafirishaji na uchukuzi na mbobezi wa usalama barabarani na Mjumbe wa Balaza la taifa la usalama barabarani na mwenyekiti wa elimu mafunzo na uenezi katika balaza hilo, akiwakumbusha madereva mambo mbalimbali muhimu yahusuyo Sheria za barabarani na somo muhimu la madereva kujitambua.
Mrakibu Msaidizi  wa Polisi Abben Swai Mkuu wa Kitengo cha Elimu Mafunzo na Uenezi wa kikosi cha Usalama wa barabarani Tanzania, akiendesha chemshabongo fupi kwa madereva wa magari ya mizigo yaendayo safari ndefu lengo ni kuwakumbusha tu kuendelea kuwa makini pindi wawapo safarini.
Mrakibu  Msaidizi wa Polisi Yoronimo Kwesibaga Saimon Mkuu wa kituo cha Polisi Bandari, akitoa salam zake wakati wa wiki ya maadhimisho ya siku ya usalama na afya barabarani.
Madereva pamoja na wageni wengine waalikwa wakiwa katika wiki ya kuelekea siku ya Usalama na Afya barabarani katika viwanja vya Impala Terminals. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...