Asasi ya Ariel Glaser Pediatric AIDS Health Initiative (AGPAHI) inayolenga kutokomeza UKIMWI kwa watoto na familia nchini Tanzania imetoa msaada wa magari mawili aina ya Nissan Patrol kwa halmashauri za wilaya za Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri hizo.

Magari hayo yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yana thamani ya shilingi milioni 186 yamenunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).

Hafla fupi ya Makabidhiano ya magari, imefanyika leo Jumatatu Novemba 5,2018 wakati wa kikao cha wadau wa afya na ustawi wa jamii mkoa wa Mwanza kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.

Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo kwa Mkuu huyo wa mkoa, Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa alisema msaada huo wa magari ni kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma za afya hususani za VVU na UKIMWI kwenye vituo vya kutolea huduma.

Dkt. Mwakyusa alisema, AGPAHI imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na halmashauri katika kuboresha huduma za VVU na UKIMWI kwa ajili ya ustawi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Magari yenye namba za usajili DFPA 7015 na DFPA 7016 yenye thamani ya shilingi milioni 186 yaliyonunuliwa na shirika la AGPAHI kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR) chini ya vituo vya Kudhibiti Magonjwa na Kinga (CDC).
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella, akikata utepe wakati wa hafla ya makabidhiano ya magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma za VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Buchosa na Misungwi mkoani Mwanza.
Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Buchosa,Crispin Luanda na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella (wa tatu kulia) wakioneshana magari yaliyotolewa na AGPAHI.
Muonekano wa magari yaliyotolewa na AGPAHI kwa ajili ya kuboresha huduma VVU na UKIMWI katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi na Buchosa.
Mkurugenzi Mtendaji wa AGPAHI, Dkt. Sekela Mwakyusa, akikabidhi ufunguo wa gari kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mheshimiwa John Mongella.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...