Wakati tarehe ya mwisho ya kupokea viongozi wa upinzani wanao omba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikifika leo hii, Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya Chama cha CUF Abdalah Mtolea amejivua uanachama wa CUF na kujiuzuru Ubunge wa Jimbo la Temeke, huku akieleza chanzo kikiwa migogoro isiyoisha katika Chama cha CUF kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Tukio la kujivua uanachama wa CUF na kujiuzuru ubunge lilitokea ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wakati akichangia hoja katika mjadala uliokuwa unaendelea mapema leo.

Ndugu Abdalah Mtolea jioni ya leo ametangaza nia yake ya kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akieleza msingi wa uamuzi huo ukiwa umejengwa katika ukweli kwamba wengi ya wapiga kura wake wamemshauri kujiunga na CCM.

Akizungumza katika kikao cha waandishi wa habari, watumishi na baadhi ya wanachama wa CCM katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, Ndugu Mtolea ameeleza sababu zinazopelekea kuomba kujiunga na CCM na kuwa amevutiwa na Mageuzi makubwa ya Kiuongozi na kazi nzuri inayofanywa na CCM na Serikali yake chini ya Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kikao hicho cha waandishi wa habari, watumishi na baadhi ya wanachama wa CCM kimehudhuriwa pia na Kamaradi Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM ambaye amemwelekeza kwenda katika tawi lililo karibu na makazi yake Wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam ili afuate utaratibu wa kuomba uanachama wa CCM.



Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Bashiru Ally akizungumza jambo wakati wa kikao cha Watumishi na baadhi ya Wanachama wa CCM,kushoto aliyekubwa Mbunge wa Temeke kwa Tiketi ya CUF Ndugu Abdalah Mtolea
  Ndugu Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM na kushoto na aliyekubwa Mbunge wa Temeke kwa Tiketi ya CUF Ndugu Abdalah Mtolea Wakifurahia Jambo
Kikao cha Watumishi na Baadhi ya Wanachama wa CCM na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Bashiru Ally Kakurwa ambacho kilipata bahati ya kupokea kauli ya Ndugu Mtolea kuomba kujiunga na CCM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...