Na Khadija Seif,Globu ya jamii  .
    
BARAZA la Sanaa Tanzania(BASATA) limewatoza faini ya Sh.milioni tatu kila mmoja Msanii Raymond Mwakyusa a.k.a Rayvanny na Naseeb Abdull maarufu Diamond pamoja na lebo ya WCB baada ya kukaidi kuufuta wimbo wao wa Mwanza kwenye Youtube.

Kwa mujibu wa BASATA ilitoa tamko kwa wasanii hao wanaotoka lebo la WCB kuufuta wimbo huo jana kabla ya saa 10:30 jioni na kutochezwa redioni na kwenye luninga lakini hawakufanya hivyo.

Katibu Mtendaji wa  BASATA Godfrey Mngereza amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa bado anasisitiza kuondolewa kwa wimbo  kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu za baraza hilo kwani ndio wasimamizi wakuu wa kazi za sanaa nchini .

Mngereza  ametoa rai kwa vyombo vyote,mitandao ya kijamii,watu ,pamoja na kumbi za starehe kutotumia wimbo huo kwani umeshafungwa rasmi toka siku ya jana.

Kwa upande wa Meneja wa Lebo hiyo ya WCB Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella amesema wamepokea taarifa hizo na kukubaliana nao kuwa ifike pahala wasanii wajue kuwa wamekosea na Basata kama wazazi au walezi wapo kwa ajili ya kurekebisha vijana na kuwalea kwa ujumla na kuwafundisha maadili mazuri kwa mustakabali ya nchini kwa ujumla.

Fella ameeleza kuwa katika kutengeneza burudani lazima kukubaliana na changamoto ili uwe imara, hivyo basi kikao cha kwanza kimeshamalizika wanasubiri  kikao kingine baada ya siku tatu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...