*Wenye maduka ya kubadilisha fedha waliokiuka sheria kukiona,leseni zao zatakiwa BoT
*Pia kuzuia kuendelea kwa ukiukaji wa sheria na kudhibiti uendeshaji wa biashara ya ubadilishaji fedha
 Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof. Florens Luoga (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya Benki Kuu kuchukua usimamizi wa Bank M Tanzania Plc (Bank M) kutokana na upungufu mkubwa wa ukwasi. Kulia ni Naibu Gavana wa Uthabiti wa sekta ya Kifedha, Dkt. Bernard Kibesse na kushoto ni Naibu Gavana wa Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila.
Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema imefanya oparesheni ya kushtukiza ya kukagua maduka ya ubadilishaji fedha na baadhi ya maduka bubu ambayo hayana leseni lakini yalikuwa yakiendesha biashara hiyo kinyume na sheria.
Operesheni hiyo iliratibiwa na Kitengo cha Ukaguzi cha Benki Kuu katika kutekeleza majukumu yake kisheria na kwamba hiyo ni oparesheni ya tatu kufanyika. 
Akizungumza leo Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania amesema uchunguzi wa kina katika miezi sita iliyopita ulibaini kuongezeka kwa biashara za kubadilisha fedha kinyume cha sheria, na kukua kwa biashara haramu ya fedha za kigeni na utakatishaji fedha, hususan kupitia maduka ya kubadilisha fedha.
Amesema BoT kupitia juhudi za Kitengo cha Ukaguzi kuwapata wahusika hazikuzaa matunda katika oparesheni mbili zilizopita. Hiyo ni kwa sababu iligundulika kuwa kuna mtandao mpana na madhubuti wa shughuli hizo na ambao ulilenga kuhakikisha kuwa shughuli za udhibiti hazifanikiwi. Baada ya mashauriano na wataalam na kushirikisha vyombo vya upelelezi na usimamizi ilionekana kuwa ili kufanikisha operesheni hiyo lililokusudiwa ni muhimu wahusika wote wadhibitiwe kwa wakati mmoja na kufanyiwa ukaguzi.
" Hii ilihitaji ushiriki wa maofisa wengi sana kutoka vyombo mbalimbali na kuhakikisha kila mahali ambapo ukaguzi uliendeshwa kuna usalama wa kutosha na Wananchi wanaarifiwa kutoingia sehemu husika kwa wakati huo. Baadhi ya washiriki katika zoezi hilo ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakiwa katika sare zao bila silaha.
"Hii ni kwa sababu siku oparesheni ilipofanyika askari wengi wa Jeshi la Polisi wapo kwenye kusimamia usalama katika vituo vya mitihani ya kidato cha pili inayoendelea," imeeleza taarifa hiyo ya BoT.Napenda kuwaarifu wananchi kuwa oparesheni hii imeisha salama na bila kuathiri mtu yeyote na tunawashukuru wananchi wa Jiji la Arusha kwa ushirikiano, hasa kwa kuwa watulivu,"amesema.
Amefafanua taratibu zinazoendelea ni za kisheria na kwamba mahojiano na wahusika yanakamilishwa na wale watakaokutwa na tuhuma za ukiukaji sheria watashughulikiwa kufuatana na taratibu za kisheria. Aidha amesema Benki Kuu inachukua hatua zifuatazo kuzuia kuendelea kwa ukiukaji wa sheria na kudhibiti uendeshaji wa biashara ya ubadilishaji fedha. Kwa takribani miezi mitatu sasa benki hiyo imesitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...