Mkuu wa kitengo cha Masoko na
Mawasialiano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na
Waziri wa Fedha na Mipango Dr Philip Mpango ( wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu
wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa ( wa pili kulia), Kaimu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Peter Msoffe (wa pili
kushoto) katika maadhimisho ya siku ya takwimu duniani iliyoadhimishwa jijini
Dodoma hivi karibuni ambapo Benki ya Exim ilitoa kiasi cha Sh Milioni 10
kufanikisha maadhimisho hayo kupitia chuo kikuu cha UDOM.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na
Mawasialiano wa Benki ya Exim Bw Stanley Kafu (katikati) akikabidhi mfano wa
hundi yenye thamani ya sh. Mil 10/- kwa
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Peter Msoffe (wa
pili kushoto) ikiwa ni mchango wa benki hiyo katika kufanikisha maadhimisho ya
siku ya takwimu duniani iliyoadhimimishwa jijini Dodoma hivi karibuni.
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip
Mpango, akizungumza na waandishi wa habari
alipohudhuria katika maadhimisho ya siku ya takwimu duniani iliyoadhimimishwa
jijini Dodoma hivi karibuni.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu (NBS), Dk. Albina Chuwa akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...