Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme
nchini (Tanesco) Dkt Alexander Kyaruzi katika akiwa kwenye picha
ya pamoja kulia kwake ni Mjumbe wa bodi ya Shirika hilo Balozi James
Nzagi na kushoto ni kwake ni Mjumbe wa Bodi hiyo Gilay Shamika
Bodi yaWakurugenziya TANESCO imesema inaridhishwa na Ubora
wa mita zinazozalishwa hapa nchini kwani zinaviwango sawan amita
zinazo zalishwa njeya nchi.
Hayo yalibainishwa leo wakati
wa ziara iliyofanywa na Bodi yaWakurugenzi hiyo katika kiwanda cha
Inhemeterna Baobab Energy System vilivyopo mjini Dar es salaam,
Mwenyekiti wa Bodi yaWakurugenziya TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi
amesema kuwa dhumuni kubwa la ziara hiyo ni kukagua na kujiridhisha na
ubora wa mita na uwezo wa viwanda hivyo katika kukidhi mahitaji ya
TANESCO na REA.
Alisema kwani kwasasa uhitaji wa Mita
umekua mkubwa kutokana na uhitaji wa umeme kwa wananchi wa Vijijini na
Mjini, pamoja na maboresho yanayofanywa na Shirika yakubadilisha mita
za wateja wa zamani ambao walifungiwa mita miaka 10 iliyopita na sasa
wanahitajika kuwekewa mita mpya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Alexander Kyaruzi kulia akiangalia mchakato wa utengenezaji wa mita katikati ni Meneja Mwandamizi wa Usambazaji na huduma kwa wateja wa shirika hilo Theodory Bayona na kushoto ni Mkurugenzi wa Kiwanda cha cha Inhemeter
Mkurugenzi wa Kiwanda cha cha Inhemeter kushoto akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) Alexander Kyaruzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...