Na Ahmed Mahmoud Arusha

BENKI kuu ya Tanzania, (BoT), imesema ina kiwango kikubwa cha fedha za kigeni kinachoweza kutosheleza kulipa madeni ya serikali na kutoa huduma zingine katika kipindi cha miezi mitano ijayo.

Hayo yameelezwa na Gavana wa Benki kuu Profesa Frolence Luoga ,alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari mjini Arusha akitoa ufafanuzi kuhusu oporesheni iliyoendeshwa Juzi na benki hiyo dhidi ya maduka ya kubadilisha fedha jijini Arusha.

Gavana,amesema zoezi hilo liliratibiwa na kitengo cha ukaguzi cha benki kuu katika kutekeleza majukumu yake ya kisheria na ni zoezi la tatu kufanyika nchini.Uchunguzi wa kina katika kipindi cha miezi sita iliyopita ulibaini kuongezeka kwa biashara ya kubadilisha fedha kinyume cha sheria na kukua kwa biashara haramu ya fedha za kigeni na utakatishaji wa fedha hususani kupitia maduka ya kubadilisha fedha.

Jambo ambalo ni hatari kwa uchumi wan chi.

Juhudi za benki hiyo kuwapata wahusika hazikuzaa matunda katika oporesheni mbili zilizopita kwa sababu iligundulika kulikuwepo na mtandao mpana na madhuhuti wa shughuli hizo ambao ulilenga kukwamisha shughuli za udhibiti .‘’Baada ya mashauriano na wataalamu na kushirikiana na vyombo vya upelelezi na usimamizi ilionekana kuwa ili kufanikisha zoezi lililokusudiwa ni muhimu wahusika wote kudhibitiwa kwa wakati mmoja na kufanyiwa ukaguzi jambo lilihitaji ushiriki wa maofisa kutoka vyombo vya dola’’.Alisema gavana .

Amesema zoezi hilo limeshirikisha askari wa jeshi la wananchi na jeshi la polisi na kuzuia watu wasiingie ndani ya maduka hayo kufanya miamala ya kifedha na zoezi hilo limemalizika salama bila kuathiri mtu yeyote.Gavana,amesema katika kipindi cha miezi mitatu ,Benki kuu imesitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha na maombi yote mapya yamesitishwa na hayatapokelewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...