Na Grace Semfuko-MAELEZO
Bunge la Jamhuri ya Watu wa China limepongeza kasi ya ujenzi wa Miradi inayofanywa na Serikali  ya Tanzania na kwamba ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania utaendelea kuimarishwa ili kuzifanya nchi hizo kuzidi kuwa na maendeleo ya kuichumi.

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang alipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni Jijini Dar Es Salaam lililojengwa na Kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering CRJE na China Major Bridge Engineering Company  ujenzi ulioanza mwaka 2012 na kukamilika April 2016.

Daraja hilo linalovuka mkondo wa maji wa Kurasini hadi Kigamboni  Jijini Dar Es Salaam lina urefu wa mita 680 na njia sita za kupitishia magari ni daraja kubwa katika nchi za Afrika Mashariki na lilizinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli April 19 mwaka 2016 na kupewa jina la Julius Nyerere kwa heshima ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Hayati  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ujenzi wa Daraja la Nyerere ulibuniwa na Serikali lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari uliokuwepo katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar Es Salaam na kurahisisha usafiri lengo ni kuwaondolea watanzania changamoto kwenye sekta ya usafirishaji.
Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defang amesema ni muda muafaka sasa kwa daraja hilo kutumika kama njia za kiuchumi kwa watu wa Tanzania.

“Nimefurahishwa na ujenzi wa Daraja hili uliojengwa na Kampuni ya CRJE ya wachina,wamefanya kazi nzuri, kwa Tanzania daraja hili ni fursa za kiuchumi kwani litarahisisha usafirishaji na kuepukana na vikwazo vilivyokuwepo awali kabla ya dara hili” alisema Cai Defang Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi ya jamii la NSSF Bw. William Erio amesema kukamilika kwa daraja hilo kumekuwa na manufaa makubwa kwa Serikali kwani limekuwa likiingizia Serikali mapato yatokanayo na kuvusha magari fedha ambazo zimekuwa zikienda kufanya shughuli zinazoinufaisha jamii ya kitanzania.

“Tunashukuru Serikali kuendelea kubuni miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo inasaidia jamii kwa asilimia mia moja,mfano daraja hili ni moja ya vyanzo vya kiuchumi kwani fedha za makusanyo hapa zinasaidia kuongeza kasi ya kuhudumia jamii kupitia ujenzi wa miradi mingine” alisema William Erio wakati akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China alipotembelea kwenye mradi huo wa daraja.
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang na watendaji wa (NSSF) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na uongozi unaosimamia huduma za daraja la Nyerere baada ya kukagua daraja hilo leo jijini Dar Es Salaam.
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang (wa katika)  akiwa ameambatana na  viongozi mbalimbali wa wakitembelea daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)
 Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la hifadhi ya jamii la (NSSF) Bw. William Erio leo alipotembelea Daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Muonekano wa Daraja kwa sasa
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...