Na Grace Semfuko-MAELEZO.

Bunge la Jamhuri ya Watu wa China limepongeza kasi ya ujenzi wa Miradi inayofanywa na Serikali  ya Tanzania na kwamba ushirikiano uliopo baina ya China na Tanzania utaendelea kuimarishwa ili kuzifanya nchi hizo kuzidi kuwa na maendeleo ya kuichumi

Hayo yamebainishwa na Makamu wa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya watu wa China Bw. Cai Defang alipotembelea Darala la Nyerere Kigamboni Jijini Dar Es Salaam lililojengwa na Kampuni ya China Railway Jiangchang Engineering CRJE na China Major Bridge Engineering Company  ujenzi ulioanza mwaka 2012 na kukamilika April 2016.

Daraja hilo linalovuka mkondo wa maji wa Kurasini hadi Kigamboni  Jijini Dar Es Salaam lina urefu wa mita 680 na njia sita za kupitishia magari ni daraja kubwa katika nchi za Afrika Mashariki na lilizinduliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli April 19 mwaka 2016 na kupewa jina la Julius Nyerere kwa heshima ya Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ujenzi wa Daraja la Nyerere ulibuniwa na Serikali lengo likiwa ni kupunguza msongamano wa magari uliokuwepo katika kivuko cha Magogoni Jijini Dar Es Salaam na kurahisisha usafiri lengo ni kuwaondolea watanzania changamoto kwenye sekta ya usafirishaji.Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti huyo wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Cai Defang amesema ni muda muafaka sasa kwa daraja hilo kutumika kama njia za kiuchumi kwa watu wa Tanzania.
 
 Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya Watu wa China Mhe. CAI Dafenga akipunga mkono wakati alipotambulishwa  Bungeni mapema leo Jijini Dodoma. Wa pili toka kulia ni Naibu Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Balozi wa China nchini Bi. WANG wa kwanza kulia. Makamu huyo wa Rais ametembelea Bunge la Tanzania akiambatana na Wabunge kumi na tano kwa lengo la kudumisha ushirikiano baina ya pande zote mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...