Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wameendesha zoezi la msako wa kuwakamata wezi wa maji ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.

Zoezi hilo linaloendelea kwa kasi limefanikisha kukamatwa kwa mkazi mmoja wa Mbezi Kati aliyetambulika kwa jina la Alhaji Londa ambaye anatuhumiwa kujiunganishia maji na kuyauza kwa wenye magari ya kubeba maji usiku. 

Akishiriki katika zoezi la Kuwasaka wezi hao, Meneja wa Mkoa kazi DAWASA Kawe, Gilbert Massawe ameweza kufanikisha kukamatwa kwa mwizi huyo anayedaiwa kujiunganishia maji zaidi ya mwaka mmoja.Katika kumbukumbu za kiofisi zinaonyesha kuwa Londa alikuwa anadaiwa Tsh. Milioni 1.8 na alisitishiwa huduma tangu mwaka jana hata hivyo alijiunganishia maji kinyemela na kuanza biashara ya kuuza maji usiku. 

Gilbert amemtaka Londa Kujisalimisha kituo cha polisi na kueleza kuwa hatua kali zitachuku dhidi yake.Baada ya DAWASA kufanya uchunguzi na kujiridhisha jana ili vamia nyumbani kwa mtuhumiwa na kukuta kweli alijiunganishia maji kama inavyoonekana pichani. 

Hatua za kisheria zimechukuliwa kwa majibu wa sheria ya DAWASA na kwa kosa hili mtuhumiwa atashitakiwa kwa makosa kadhaa ikiwemo wizi wa maji, uharibifu wa miundombinu ya maji na uhujumu uchumi.
Meneja wa Mkoa kazi wa DAWASA Kawe Gilbert Massawe (kulia) akishiriki katika operesheni ya kumkamatamkazi mmoja wa Mbezi Kati aliyetambulika kwa jina la Alhaji Londa ambaye anatuhumiwa kujiunganishia maji na kuyauza kwa wenye magari ya kubeba maji usiku. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...