Rais Mstaafu awamu ya nne Dkt. Jakaya  Kikwete amesema kuwa  taasisi yake pamoja na kitabu chake cha The Journey Of My Life,ni vitu alivyofikiria kuvianzisha,viwe kumbukizi kabla ya kumaliza uongozi wake akiwa kama Rais.

Dkt. Kikwete ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla maalum ya Chakula cha jioni iliyoandaliwa na Chemba ya Biashara ya Marekani hapa nchini (AMCHAM), kwa lengo la kuishukuru Serikali ya Tanzania.

Amesema katika uongozi wake marafiki  walifikiri jambo ambalo atalifanya mara baada ya kumaliza utumishi wa umma aliohudumu kwa miaka 40, ambapo alitaka kuweka uzoefu na mawazo yake katika maandishi ili yasiweze kufutika.

Kikwete amesema katika kitabu cha The Journey of My Life  ameeleza kuhusiana na taasisi ya Jakaya na maisha yake tangu akiwa mdogo huko kijijini Msoga pamoja na uzoefu wa uongozi kwa miaka 40,amesema katika kitabu chake amegusia maeneo mbalimbali yakiwemo kilimo, afya, vijana na utawala.

Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania  Dkt. Inmi Patterson amempongeza Dkt. Kikwete kwa uthubutu na amewashukuru watanzania kwa ukarimu, upendo na ushirikiano pamoja na kutunza amani hapa nchini.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo kuhusu historia ya maisha yake pamoja na uanzishwaji wa Taasisi ya Dkt Kikwete katika hafla ya iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania  Dkt. Inmi Patterson akitoa shukrani kwa mchango pamoja na mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Marekani katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka MMG)

Sehemu ya wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwa katika hafla hiyo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwanzilishi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete Dkt. Jakaya  Kikwete(kulia) akioneshwa moja ya Picha na Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Marekani hapa nchini (AMCHAM) Garry Friend (kushoto) iliyotoka Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ikiashiria kutambua mchango wa Serikali ya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...