Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) ameahidi kushirikiana na watumishi wa ofisi yake kupanga mikakati endelevu itakayowezesha kutoa huduma bora kwa umma na kuhakikisha ofisi hiyo inakuwa na mtazamo chanya katika kuwahudumia wananchi.

Dkt. Mwanjelwa ametoa ahadi hiyo leo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. Dkt. Mwanjelwa ameomba ushirikiano wa dhati kutoka kwa watumishi wa ofisi yake kwani kila mtumishi ana mchango na umuhimu wake katika kuboresha utuoaji wa huduma kwa umma.

Aidha, Dkt. Mwanjelwa amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri mwenye dhamana ya utumishi na utawala bora.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 10 Novemba, 2018 na kumuapisha tarehe 12 Novemba, 2018.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. 
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi.Dorothy Mwaluko, akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi, mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary M. Mwanjelwa (Mb) akisalimiana na mmoja wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...