NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

UMOJA na kufanyakazi kwa ushirikiano miongoni mwa Watendaji na Madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Kaliua ndio sababu ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye mtihani wa darasa la saba , afya na ukusanyaji mapato mkoani Tabora.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Dkt. John Pima wakati wa kikao cha robo ya kwanza cha Baraza la Madiwani baadaya Watendaji wake kupongezwa kwa uchapaji kazi mzuri.Alisema kufanya vizuri katika matokeo ya kumaliza elimu ya msingi na kuwawezesha kuwa wa kwanza kimkoa na kutoa mwanafunzi bora wa kiume kitaifa na kuwa wa nne kitaifa katika ukusanyaji wa mapato na kushika nafasi ya nne kitaifa ni sababu ya uwepo wa mshikamano kati yao na Madiwani.

Dkt. Pima aliongeza kuwa hata kule kufanya vizuri katika mpango wa afya wa RBF na kuifanya Halmashauri hiyo kushika nafasi ya kwanza kimkoa ni sababu ya ushauri kutoka Kamati ya Elimu , Afya na Maji.Alisema wao kama watendaji wataendelea kupokea ushauri mzuri kwa ajili ya kuendelea kulinda nafasi waliyopata.Kuhusu Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mitihani yake ya kumaliza Darasa la Saba , alisema wataendelea kuwa naye karibu ili aendelee kufanya vizuri kwa ajili ya kuwa kioo cha Kaliua.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua Haruna Kasele alisema Baraza la Madiwani linawapongeza Watendaji wote waliofanyakazi kwa bidii na kuiwezesha Halmashauri hiyo kufanya vizuri kimkoa katika elimu na kiafya na kuwa wa nne kitaifa katika ukusanyaji mapato.Aliagiza Watendaji katika Idara zilizofanya vizuri ni vema wakapongezwa na kupewa cheti kinachotambua mchango wao uliong’arisha Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua katika maeneo hayo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kaliua Magalena Sakaya alitaka kuanzishwa kwa zoezi la kuwashindanisha watumishi na wakuu wao wa idara katika Halmashauri ya Kaliua ili wanaofanya vizuri wapongezwe na wanaofanya vibaya warekebiswe ili kuendelea kuifanya Kaliua iwe ya kwanza sio tu kwa ngazi ya Mkoa hata kitaifa. 
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kikao kilichokuwa kikijadili taarifa za utekelezaji wa robo mwaka kilichofanyika jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...