MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema ipo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ‘syllabus’ ya elimu nchini ili wanafunzi waanze kufundishwa maana ya kodi tangu wakiwa wadogo.

Hatua hiyo inatokana na kuwapo kwa uelewa mdogo katika masuala ya kodi ambao unachangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wengi hasa wanaoanzisha biashara kuona ulipaji kodi ni mzigo.

 Akizungumza katika mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Rose Mahendeka alisema mchakato huo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzanian Associate kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel and Fernandes Communications, yalilenga kuwakuelimisha jamii kuhusu masuala ya kodi. Aidha, Mahendeka alisema bado kuna changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutoelewa umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi katika biashara zao.

“Wafanyabiashara wengi hawana uelewa wa kodi ila tupo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ya elimu waanze kupata wakiwa wadogo kabisa kule mashule ili waanze kupata uelewa wakiwa wadogo kabisa kwamba nini maana ya kodi, inahusu nini na jinsi gani kodi inalipwa Tanzania, tunaamini kwa njia hiyo watu wengi wataelewa,” alisema.


Afisa Elimu Mkuu kwa mlipa kodi kutoka TRA, Rose Mahendeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara, Kwigaya Mito akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Abel & Fernandes Communications, Fatma Fernandes akizungumza katika warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzania Associates kwa lengo la kuwaelimisha wafanyabiashara wa kati na wadogo kuhusu sheria za kodi na umuhimu wa kulipa kodi.
Mshauri wa masuala ya Kodi, Petro Francis akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa Taasisi ya The Tanzania Associates kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.
Mwanzilishi wa Taasisi ya The Tanzania Associates, Lucy Minde akichangia mada katika warsha iliyoandaliwa taasisi hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel & Fernandes Communications kwa lengo la kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa kisheria kuhusu umuhimu wa kulipa kodi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...