Na Francis Godwin,Iringa

MWENYEKITI  wa  bodi ya  shirika la  umeme Tanzania  (TANESCO )  Dkt   Alexander Kyaruzi amesema  kuwa  hali ya  uzalishaji  wa  umeme  nchini  ni  nzuri na  kuwa   watanzania  wasitegemee  kuwepo  kwa mgao   wa  umeme  kwa  mwaka  huu.

Akizungumza  wakati  wa   hafla ya  uwashaji  umeme  kijiji  cha  Ndolezi katika  Halmashauri ya  mji Mafinga  Dkt  Kyaruzi  alisema  kuwa  pamoja na  kuwa  kipindi cha  kiangazi  kinakwenda  kumalizika ila hali ya maji  katika  vituo  vya uzalishaji  umeme  vya Kidatu na Mtera  ni  nzuri  na kuwa maji hayo yataendelea  kuongezeka  zaidi kwani msimu wa masika  unakaribia.

Kuhusu   kasi ya  usogezaji wa  umeme  katika  vijiji  ,vitongoji  na  maeneo ya  visiwa alisema  kuwa  kasi  inaendelea   vizuri na  kuwa  hadi  mwaka 2021  maeneo  yote ya  nchi umeme  utakuwa  umefika na  hakutakuwa na kijiji  wala  kisiwa  ambacho  wananchi  watakuwa  hawana  umeme .

Pamoja na  umeme    huo  wa maji na  gesi  ambao  unatumika  kwa sasa bado  alisema  shirika  limeendelea  na uvumbuzi  wa  vyanzo  vingine  vya  umeme kama  umeme wa  joto ardhi  ambao tafiti  zinaonyesha  baadhi ya  mikoa kama  mkoa  wa Mbeya  kuwepo  kwa  umeme   huo .

"  Tunategemea  miaka  mitano mbele  kuwa na umeme  utakaozalishwa   kupitia  joto  ardhi   hivyo  bado  nchi  itaendelea  kuwa  na  uhakika  wa  umeme baada ya  kuwa na  vyanvyo  tofauti  tofauti "  alisema  Dkt  Kyaruzi

Alisema  kuwa maeneo    Ziwa  ngozi  mkoani  Mbeya  ni  eneo la kwanza  ambalo  wamefanikiwa  kufanya  utafiti na  kuonekana  lina weza  kuzalisha  umeme  wa  joto  ardhi na  tayari  wamempata  mkandarasi  wa kufanya  zoezi la  uchimbaji  wa eneo hilo .
 Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Ali  Hapi mwenye  suti  nyeusi na mkurugenzi wa bodi ya Tanesco Dkt Alexander Kyarusi kulia  wakiwasha  umeme  kijiji cha Ndolezi Mafinga mkoani Iringa
 Mkuu wa  mkoa wa Iringa Alli Hapi  akisikiliza kero za  wananchi juu ya umeme wilayani Mufindi jana
 Mwenyekiti wa  bodi ya Tanesco Dkt Alexander Kyaruzi (kushoto) akifuatilia taarifa ya meneja wa Tanesco Mafinga  wakati wa uwashaji  umeme kijiji cha Ndolezi
Wananchi Mufindi wakitoa kero zao kwa  mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi  wakati wa  kuwasha umeme kijiji cha Ndolezi Mafinga.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...