Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inawafahamisha wanafunzi wote wa taasisi za elimu ya juu kuwa leo, Jumatano, Novemba 21, 2018 imeanza kupokea rufaa za mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kwa kwa njia ya mtandao.

Dirisha la kuwasilisha rufaa hizo litakuwa wazi kwa siku tano, kuanzia leo hadi Jumapili, Novemba 25, 2018 na linapatikana kupitia http.olas.heslb.go.tz. Wanafunzi watakaokua wametimiza masharti na sifa watapangiwa mikopo kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Novemba, 2018.

HESLB imefungua dirisha hili ili kutoa fursa kwa wanafunzi wahitaji ambao hadi sasa hawajapata mkopo au hawajaridhika na kiwango cha mkopo walichopangiwa, kuwasilisha maelezo na nyaraka kuthibitisha uhitaji wao. Maelekezo ya kina kuhusu namna ya kuwasilisha na nyaraka zinazohitajika yanapatikana kwenye mtandao (http.olas.heslb.go.tz).

Ili kuwasilisha taarifa na nyaraka zake za rufaa, mwanafunzi anapaswa kufungua mtandao huo, kusoma maelekezo na kutumia namba yake ya mtihani wa kidato cha nne aliyoombea mkopo kwa mwaka huu (2018/2019) kuingia na kuwasilisha taarifa zake kwa njia ya mtandao tu.

Hadi leo (Jumatano, Novemba 21, 2018), jumla ya wanafunzi 37,969 wa mwaka wa kwanza wamepangiwa mikopo na wanaendelea na masomo katika taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini.

Katika mwaka huu wa masomo, Serikali imetenga TZS 427.5 bilioni kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu ambazo zitawanufaisha wanafunzi zaidi ya wanafunzi 120,000wakiwemo 83,000 wa mwaka wa pili, tatu na kuendelea waliopo vyuoni ambao wamefaulu mitihani yao ya mwaka.

Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
DAR ES SALAAM
JUMATANO, NOVEMBA 21, 2018

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...