Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) imekutana na wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Akizungumza leo Dar es Salaam na wanafunzi hao katika chuo hicho Meneja wa Upangaji Mikopo wa Bodi hiyo Julitha Miyedu amesema kuwa taratibu za kuomba mikopo ziko wazi kutokana na vigezo na masharti vilivyoanishwa na kwamba bodi hiyo ipo kwa ajili ya wanafunzi kwa lengo la kuhakikisha kila mwenye vigezo vya mikopo anapata kwa wakati ili kuwezesha wanafunzi wasifikirie suala fedha katika kufanya mahitaji.

Miyedu elimu wanayoitoa ya mikopo ni endelevu katika kuhakikisha kila mwanafunzi anapata uelewa wa bodi inavyochakata mikopo kwa wanafunzi kwa kutumia vigezo vilivyoainishwa.“Haachwi mtu kwenye suala la utoaji mikopo ikiwa nia ya bodi kuona kila mtu anapata mkopo kutokana vigezo vilivyoanishwa katika kuijenga nchi yetu na mikopo huyo kwa wanuifaka baada ya kuhitimu kurejesha kwa ajili ya kunufaisha wengine ”amesema Miyedu.

Kwa upande wake Ofisa  Mawasiliano Mwandamizi wa Bodi ya Mikopo Veneranda Malima amesema wanafunzi wanatakiwa kusoma vitu katika mitandao na vipeperushi vya bodi kwa kupata taarifa zinazotokana na bodi. Amesema kuwa bodi imeweka mfumo wa kielekroniki katika kurahisisha malipo ya mikopo kwa wanafunzi kupitia kwa maafisa wa mikopo wa chuo na ndio inakuwa karibu nao kwa kila masuala ya wanafunzi yanayohusiana na mikopo huku akisisitiza bodi kuendelea kutoa taarifa katika utaratibu uliozoeleka, hivyo wanafunzi wajiepushe na kupata taarifa katika sehemu zisizo rasmi

Afisa Mikopo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM); Lugano Mwakyusa akitoa ufafanuzi wamasuala ya Wanafunzi waliojiunga na chuo hicho.

Katibu wa serikali ya Wanafunzi waChuo Kikuu cha Dar es Salaam, Respicious Reginald akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Meneja wa Utoaji Mikopo, Neema Nitume akitoa ufafanuzi wa masuala malipo ya Fedha za mikopo kwa Wanafunzi wanaonufaikana mikopo ya elimu ya juu.

Maafisa waandamiziwa HESLB wakiwa na viongozi wa DARUSO baada ya kuanza kwa mhadhara kwa Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa kulia mstari wa mbele ni Waziri Mkuu wa DARUSO, Paul Goodluck, kulia kwake ni Waziri wa mikopo, LigwaDictaeakifuatiwa na AfisaMawasiliano wa HESLB Veneranda Malima na Menejawa Utoaji Mikopo, Neema Nitume.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...