Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Bonde la Wami/Ruvu linatarajia kuwafikisha wamiliki hoteli 100 kutokana na kushindwa kulipa Maji ya visima walivyovichimba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa wa Maji Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani amesema watafungulia mashitaka Novemba 21 kutokana na kushindwa kulipa maji wanayoyatumia katika visima walivyovichimba.Amesema wamekuwa wakifanya mazungumzo na mwisho hakuna matokeo ya ulipaji wa visima hivyo na kuamua kwenda mahakamani.Ngonyani amesema wamiliki wa hoteli 100 wamekuwa wakaidi kuhusiana na ulipaji wa ada ya maji wanayoyatumia.

Aidha amesema kuwa kutokana ulipaji huo uko kisheria sehemu yao ya kwenda kulipia.Amesema kuwa hakuna mtu atakayeachwa salama katika matumizi ya maji ambayo yako kisheria labda hiyo sheria haipo na kama ipo lazima watalipa ili fedha hiyo iendelee kutinza vyanzo vya maji.

"Bonde la Wami/Ruvu litaendelea kusimamia vyanzo vya maji kuhakikisha vinalindwa kwa vizazi vilivyopo na vijavyo hivyo hakuna mtu anayeonewa"amesema Ngonyani.Amezitaja baadhi ya Hoteli zitakazofunguliwa mashitaka mahakamani ni Kebbs Hoteli,Lamada Hoteli, Ubungo Plaza, King Gulf, New Land Hoteli, Flex Hoteli, Rungwe Palace,Roland Hoteli,Luch Time,Saneth Hoteli,pamoja na New Laki.

Ngonyani ,Amesema kuwa kampuni 25 wamepewa notisi ya kuchepusha na kutumia maji kinyume cha sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za maji.Alizitaja baadhi kampuni hizo ni GSM Mall, Farm Equip,Man Trac, Sido Regional, Tol Gases, St.Mary's International School, Dar Group Hospital pamoja na Tarmal Industries Ltd..

Hata hivyo kampuni 25 za mafuta zimepewa notisi ya uchepushaji maji na kutumia kinyume cha sheria.Baadhi ya Kampuni hizo ni PetroAfrica ,State Oil,Meck one Industry,Kobil, Victoria,TSN,Oil Com,Puma,JM Energy Maunt Meru, Lake Group(Lake Oil),GTL Group,Mogas, GBP.
Afisa wa Maji wa Bonde la Wami/Ruvu  Simon Ngonyani akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na watumiaji wa Maji ambao hawafuati sheria katika ofisi za Maji Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...