Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo amekemea mila ya wafiwa kutakaswa kwa kufanya tendo la ndoa na mtu mwingine ili kuondoa mkosi kwenye kisiwa cha Ukara kwa kuwa wanaweza kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU) na ugonjwa wa Ini. 

Waziri Jafo amekemea tabia hiyo inayoendelea kisiwani humo kwasasa baada ya watu wengi kufiwa na wenza wao kutokana na ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama miezi michache iliyopita na kupoteza watu wengi.

Katika ziara yake maalum ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli la ujenzi wa majengo yenye hadhi ya hospitali katika eneo la Ukara, Waziri Jafo amesema zoezi hilo limeanza rasmi leo na kuagiza ujenzi huo ukamilike ndani ya miezi mitatu. Amesema amepata taarifa kwamba wafiwa wanafanya mapenzi na watu wengine ili watolewe mikosi kitendo ambacho ametahadharisha kwamba kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo kutokana na watu wao kuambukizwa nagonjwa yakiwepo gonjwa la UKIMWI na Ugonjwa wa Ini yaani Hepatitis B.

Jafo amewataka wale ambao bado hawajafanya kitendo hicho cha kutakaswa wasijaribu kabisa kwani kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela amemuhakikishia waziri Jafo kwamba watasimamia ipasavyo ujenzi huo na kukamilika ndani ya miezi mitatu ili adhima ya Rais Magufuli ya kuwasaidia wananchi wa Ukara katika sekta ya afya iweze kutimia.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akiwa na viongozi wenzake wakishiriki na wananchi kushusha vifaa vya ujenzi kutoka katika meli kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali kisiwa cha Ukara.
2
.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akitoa maagizo viongozi wa Mwanza.
3
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akizungumza mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo
4
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali wakielekea kisiwa cha Ukara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...