Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Watu sita wanaodaiwa kumuua aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dr. Edmund Sengondo Mvungi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shtaka la mauaji.
Washtakiwa hao ambao wamesomewa shtaka hilo Leo Novemba 22. 2018 na wakili wa Serikali Lilian Rwetabula mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Agustina Mbando kuwa ni, Msigwa Matonya(35), Mianda  Mlewa(45), Paulo Mdonondo(35), Longishu Losindo(34), Juma Kangungu(34) na John Mayunga(60).
Katika kesi hiyo, mpya ya mauaji namba 6, 2018,  washtakiwa hao wameshtakiwa kwa kosa la mauaji ya kukusudia  kinyume na kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mapema leo asubuhi, washtakiwa hao waliachiwa mbele ya Jaji Sam Rumanyika wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada upande wa mashtaka kuwasilisha ombi la kuindoaa kesi hiyo chini ya kifungu cha 91(1) cha sheria ya makosa ya jinai (CPA). 
Hatua hiyo imefikwa baada ya wakili wa  Serikali Nassoro Katuga kuiomba mahakama kufuta kesi hiyo kwa kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi  ya washtakiwa.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili Lilian amedai, Novemba 3 mwaka 2013 huko Kibwerenge Msakuzi eneo la Mbezi, washtakiwa walimuua Dr Mvungi. Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji

Kabla ya kuahirishwa kesi hiyo, wa shtaka hao walidai kuwa, hiyo siyo kesi mpya,  llikuwa inaendelea kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu mbele ya Jaji Sam Rumanyika lakini upande wa mashtaka wameamua kuindoa na kuileta upya hapa Kisutu.
Pia washtakiwa hao wameiomba mahakama iwaeleze upande wa mashtaka wakamilishe upelelezi kwa haraka kwani hakuna chochote kipya kwa sababu hakuna ushahidi mpya zaidi ya ule ule uliosomwa kwenye Committal( maelezo ya mashahidi). Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 6, 2018 kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
  Watuhumiwa sita wanaodaiwa kumuua aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dr. Edmund Sengondo Mvungi wakitoka mahakamani  baada ya kusomewa mashatka yao leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

   Watuhumiwa sita wanaodaiwa kumuua aliyekuwa mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba Dr. Edmund Sengondo Mvungi wakitoka mahakamani  baada ya kusomewa mashatka yao leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...