Shirikisho la Mpira wa kikapu nchini (TBF) linapenda kuutaarifu umma kuwa kutakuwa Mafunzo kwa ajili ya kusaka Vipaji na Kuendeleza Vipaji kwa vijana wanaoshiki Mchezo wa Mpira wa kikapu hapa Nchini Tanzania.

Kocha wa Timu ya Taifa wa Mpira wa Kikapu Matthew McCollister pamoja na Msaidizi wake Kocha Steven Michael Priestley wataingua Nchini leo tarehe 2/11/2018 kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro toka Marekani.

Kocha huyo anakuja kwa mara ya pili nchini Tanzania, kwa mara ya kwanza akija na baadhi ya wachezaji nguli wa zamani wa mchezo huo wa kikapu na kutoa mafunzo kwa vijana mbalimbali.

Mafunzo yatakuwa kwa Vijana wote wenye umri kuanzia miaka 10 hadi 20, Mafunzo yamegawanyika sehemu mbili kama inavyo elekeza hapa chini
a) Arusha Kuanzia tarehe 3- 5 November 2018 Viwanja vya Soweto na Sheikh Amri Abedi
b) Dsm Kuanzia tarehe 7-8 November Viwanja vya JMK Pack kidongo Chekundu.
c) Muda wa Mafunzo ni kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 na Baadaye saa 9 hadi saa
11 jioni.

Shirikisho linapenda kuwakaribisha Vijana wote pamoja na mikoa jirani ili tuweze kupata fursa ya mafunzo kupitia Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, katika Maeneo niliyo eleza hapo juu.
Pia Shirikisho linapenda Kuwa karibisha Wazazi wote ili waweze kuwapa Moyo vijana wetu wakati wa mafunzo haya endelevu ili kuwajengea uwezo vijana wetu wawe wachezaji wazuri kwa Taifa letu.

Pia Shirikisho linawaomba wadau wote kutoa ushirikiano katika Mafunzo haya kwa Vijana wetu katika kuhakikisha mchezo wa mpira wa kikapu unarejesha heshima yake kitaifa na kimataifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...