Na Saidina Msangi na Farida Ramadhani-WFM.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema kuwa Serikali itazingatia maoni na ushauri wa wabunge wote katika Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.

Waziri Mpango alitoa kauli hiyo Bungeni wakati akiahirisha mjadala wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2019/2020.

Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maoni ya wabunge kuhusu kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kuongeza bajeti ya kilimo, Dkt. Mpango alisema kuwa uongezaji wa bajeti ya kilimo ni muhimu lakini lazima ufanyike kwa ulinganifu wa mahitaji ya kibajeti ya sekta nyingine muhimu.

“Ni muhimu kukumbuka kuwa sekta ya kilimo ina mwingiliano mkubwa na sekta nyingine. Mwenendo bora wa kilimo unategemea sana uwekezaji wa sekta saidizi hasa miundombinu ya umwagiliaji, barabara vijijini, umeme kwa ajili ya kuendesha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, uzalishaji wa zana za kilimo, dawa, elimu na afya kwa wakulima” alisema Waziri Mpango.

Aidha, waziri Mpango aliongeza kuwa ni muhimu kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika sekta za kilimo na uvuvi, kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi pamoja na kutafuta masoko ya kikanda na kimataifa.Akizungumzia miradi mikubwa inayotajwa kukwama Waziri Mpango alifafafanua kuwa miradi iliyokwama imetokana na masharti hasi ya wawekezaji ambayo hayana maslahi kwa Taifa.
 Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma.
 Viongozi waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mjadala wa wabunge, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA- Bw. Charles Kichere (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (wa pili kushoto) na Viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mjadala wa wabunge, kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala wa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maadalizi ya Mpango na Bajeti ya Mwaka 2019/2020, Jijini Dodoma jana.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...