Wataalam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wataalam wa afya wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Mtwara, Ligula wanaendelea kutoa huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wa mkoa huo ikiwemo huduma za kibingwa ambazo awali hazikuwahi kufanyika hospitalini hapo.

Moja ya huduma za kibingwa zilizofanyika leo ni kuchukua sampuli ya uvimbe uliokua ndani ya ini kwa kutumia sindano wakiongozwa na mashine ya Utra sound. ‘’Mgonjwa huyu tumemfanyia kipimo cha sindano (FNAC) kwa kuongozwa na mashine ya Utra sound lengo ni kufanya uchunguzi zaidi ili mgonjwa aweze kupata tiba sahihi’’. Amesema Dkt. Mosha.

Maeneo mengine ambayo watalam wametoa huduma ni pamoja na magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho, watoto, magonjwa ya koo, pua na masikio, maabara pamoja na magonjwa ya ndani.

Utoaji wa huduma hizo unaenda sambamba na kuwajengea uwezo watalaam wa Hospitali ya Ligula ili kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Daktari Bingwa wa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ya binadamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Innocent Mosha (kushoto) kwa kushirikiana na mtaalam wa Radiolojia Dkt. Maria Mtolera wakichukua sampuli ya uvimbe uliokua ndani ya ini kwa kutumia sindano wakiongozwa na mashine ya Utra sound. 
Daktari Bingwa kutoka Muhimbili Judith Mwende akifanya upasuaji wa mtoto wa jicho leo katika Hospitali ya Ligula. 
Wataalam wa afya wa MNH kwa kushirikiana na watalaam wa afya wa Hospitali ya Ligula wakimfanyia upasuaji mgonjwa mwenye matatizo ya magonjwa ya kike na uzazi. 
Daktari Bingwa wa upasuaji wa pua, koo na masikio kutoka Muhimbili Willybroad Massawe (kulia) akimuhudumia mgonjwa mwenye tatizo la sikio. 
Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara ambao wamejitokeza leo kwa ajili ya kupata huduma za afya, ushauri na matibabu mbalimbali. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...