Na Khadija Seif,Globu ya Jamii.
Mafunzo ya elimu ya kutokomeza biashara haramu ya usafirishaji binadamu yafunguliwa rasmi jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na majaji wa nchini Tanzania pamoja na wawakilishi kutoka nchi ya Afrika Kusini na Marekani.

Mafunzo hayo ya siku tatu yataendeshwa na Wizara ya Mambo kwa majaji wa Nchini Tanzania, na wawakilishi kutoka Afrika Kusini na Marekani.

Jaji Mfawidhi wa  Mahakama Kuu ya Tanzania Beatrice Mutungi ameeleza lengo la mafunzo hayo kupatiwa kwa majaji ili kupunguza kasi na kutokomeza biashara hiyo haramu ya usafirishaji binadamu.

Jaji Mutungi amesema kuwa waashiriki hao wametoka sehemu mbalimmbali nchini  ambao ni  hakimu mkazi kutoka mikoani kama Arusha,Tanga,Lindi,Mtwara,Iringa na Dar es salaam na kuwapa fursa ya kupata uelewa mkubwa zaidi ili kutoa adhabu na hukumu ambazo zitastahili kwa watuhumiwa wanaojihusisha na biashara hizo haramu.

Mutungi amefafanua kwakina kuwa biashara hizo zinaambatana na uongo ambao unaowafanya walezi au wazazi wa vijana kutoa ruhusa kwa vijana wao  kwa wafanyabiashara hiyo haramu na kutoa ahadi za kuwasomesha wakifika mijini  na wakifika mambo hubadilika na kufanyiwa biashara za usiku za mabaa, na wengine kufanyishwa biashara ya kuuza mwili (uchangudoa)

Alikadhalika Mutungi amewapongeza washiriki wote na anatumaini elimu hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na kutokomeza biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

Hata hivyo serikali inaendelea na mikakati ya kukamatwa maharamia wote wa ndani na nje ya nchi kwani ndio wanaoendelea kuumiza nguvu kazi ya  Taifa.

Mwenyekiti wa Kuzuia na Kupamabana na biashara haramu ya usafirishaji binadamu ADASTUS MAGERE amesema mafunzo hayo yamekuja kipindi hiki kutokana na kushamiri kwa kesi nyingi za mauaji,mimba za utotoni,utekaji.

Magere amewaambia watanzania kuwa licha  ya mimba za utotoni bali pia wasichana pamoja na  wavulana wa umri mdogo wamekua wakihamishwa vijijini kwenda mijini kwa ajili ya kutumiwa Kwenye biashara haramu kama kujihusisha na uchangudoa, uhalifu ikiwemo ujambazi.

Kutokana na biashara hiyo haramu kunawanyima vijana wengi haki zao za msingi kwani wengi wana umri mdogo ambapo wangekua mashuleni na vitendo hivo vinatokea kutokana na umasikini kwa jamii na familia zao kutokumudu gharama za kimaisha na kulazimika vijana wadogo kutafuta maisha sehemu zingine na hata nje ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...