Ma- Masters wa Karate toka mitindo tofauti walihudhuria ufungaji wa sherehe ya chama cha Jundokan kilichotimiza miaka 65 na kuwakusanya wanachama wake toka nchi 30 ikiwemo na Tanzania iliyowakilishwa  na sensei Fundi Rumadha kwenye Asato Royal Orion Hotel, Naha,Okinawa,Japan. 
 Meza kuu magwiji wa karate ngazi ya juu kabisa wa Jundokan So Honbu.Masters: Kancho Yoshihiro Miyazato mwenyekiti wa Jundokan pia ni mtoto wa Eiichi Miyazato, Yasuda sensei, Kinjo sensei, Gima sensei, Higa sensei, Nakada sensei(USA), Renee sensei(France), Merriman sensei(USA) na Gsodam sensei ( Austria).
 Sensei Rumadha Fundi akiwa na Meitatsu Yagi kulia  wa  Meibukan Goju Ryu ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mwanafunzi wa Chojun Miyagi sensei, Meitoku Yagi mwanzilishi wa Meibukan Goju Ryu, kati ni master wa Okinawa Kobudo.
 Master Tetnosuke Yasuda Dan 10, umri wa zaidi miaka 94 akiwa na sensei Fundi Rumadha
 Sensei Rumadha akiwa Mwenyekiti wa Jundokan ambae pia ni mtoto wa mwanzilishi wa chama hicho master Eiichi Miyazato, pia ndie aliyekuwa mwalimu wa sensei Bomani mwanzilishi wa tawi la Jundokan Tanzania 1973.
Katika ufungaji wa sherehe hizo, pia walitunukiwa shahada au Dan wale wote waliopita mitihani yao asubuhi kabla ya sherehe. Ngazi ya juu kabisa katika shere hii kutunukiwa Dan,  ni Master Rony Kluger toka Israel aliyefuzu na kupewa shahada ya dan ya 9 na kuwa na cheo cha "Hanshi". pichani hapo Master Kluger akifanya kata ya Tensho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...