Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa nafasi ya Mwisho kwa Mshtakiwa Peter Msigwa ambaye in Mbunge wa Iringa Mjini kutafuta wakili wa kumtetea katika kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na viongozi wenzake nane wa Chadema ma sivyo, Mahakama itaendelea na usikilizwaji wa kesi hiyo bila uwepo wa wakili wake.

Msigwa pia ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anatukanwa Kisheria na mawakili wa upande wa mashtaka kwa sababu mawakili wake wanajitoa kumtetea.Hatua hiyo imefikwa leo Novemba 12. 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kwa usikilizwaji wa upande wa mashtaka ambao walidai mahakamani hapo kuwa wako tayari kwa kuendela na hatua hiyo na kwa leo walikuwa na shahidi mmoja.

Msigwa amepewa nafasi hiyo ya mwisho baada ya wawakili wake wawili waliokuwa wawili waliokuwa wakimtetea kujitoa kwa madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi.Mchungaji Msigwa ameeleza hayo baada ya wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi kudai kuwa inaonekana Msigwa amepanga njama ili mawakili wake wajitoe.

Kutokana na hatua hiyo, Msigwa alisimama na kueleza kuwa anaona Wakili wa Serikali kama anamtukana kisheria na kumnyanyapaa."Hakimu wewe ni shahidi mawakili wangu wamejitoa kwa sababu ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi, wakili wa serikali hana haki wala haimuhusu kuhusu mawakili wangu,"ameeleza.Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri amesema ni haki ya Kikatiba kwa mshtakiwa kuwakilishwa na Wakili, lakini anatoa nafasi ya mwisho kwa Msigwa na akishindwa ataonekana amefanya makusudi na kesi itaendelea bila ya yeye kuwa na wakili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...