Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kupeleka huduma bora za kimaendeleo kwa wananchi wote nchini.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa barabara iliyojengwa kwa kiwango cha lami ya Bonite yenye urefu wa kilometa 2.93 iliyopo katika Manispaa ya Moshi. 
Makamu wa Rais yupo mkoani Kilimanjaro kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
“Nawapongeza kwa Usafi na nawapongeza kwa miundombinu ya ndani katika Manispaa ya Moshi, Serikali yetu inaleta maendeleo kwa kila Mtanzania” alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais anaendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro ambapo pamoja na kufungua barabara ya Bonite pia aliweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Pasua ambacho kimegharimu shilingi za Kitanzania milioni 400 na kitakuwa na Wodi ya Mama na Mtoto, Chumba cha Upasuaji, Xray na Maabara.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema ndani ya miezi 18 Vituo vya Afya 350 vinategemea kukamilika na kwa mwaka wa fedha 2018-2019 hospitali mpya 67 za wilaya zitajengwa ambapo katika Mkoa wa Kilimanjaro Wilaya ya Rombo na Siha zitajengwa hospitali hizo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ufunguzi wa barabara Bonite yenye urefu wa kilomita 2.93 iliyojengwa kwa kiwango cha lami wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira(katikati), Meya wa Manispaa ya Moshi Ndugu Raymond Mboya (kulia)  Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ndugu Kippi Warioba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (kushoto).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa barabara ya Bonite yenye urefu wa kilomita 2.93 iliyopo Moshi Manispaa.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Meya wa Manispaa ya Moshi Ndugu Raymond Mboya wakati wa kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa barabara ya Bonite yenye urefu wa kilomita 2.93, wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira(katikati),Mkuu wa Wilaya ya Moshi Ndugu Kippi Warioba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo (kushoto). (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...