NA Estom Sanga- DSM

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr. Hafez Ghanem amefanya ziara katika mtaa wa Mamboleo,halmashauri ya wilaya ya Temeke jijini DSM na kukutana na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

Akizungumza na Walengwa hao baada ya kukagua bidhaa wanazozitengeneza kama njia mojawapo ya kukuza kipato chao, Dr. Ghanem amesema jitihada waliyonyesha Walengwa hao ya kuuchukia Umaskini ,itaendelea kuungawa mkono na Benki hiyo ya Dunia ambayo amesema ni rafiki mkubwa wa Serikali ya Tanzania.

Dr.Ghanem ametoa rai maalum kwa Walengwa hao wa TASAF kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji mali na kutumia mazingira mazuri ya kujiletea maendeleo kwani amesema ni dhahiri kuwa serikali ya Tanzania inawajali na imeonyesha utayari wa kuboresha maisha ya wananchi. Aidha Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika ambaye aliambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo Bi. Bella Bird, amesisitiza kuwa taasisi hiyo kubwa ya fedha Duniani itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kufadhili Mpango huo wa Kunusuru Kaya Maskini kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha utekelezaji wake.

Akizungumza kwenye Mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bw. Ladislaus Mwamanga ameelezea mafanikio makubwa ambayo Mfuko huo umepata tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 18 iliyopita hususani katika nyanja za elimu,afya,maji, na uchumi. Bw. Mwamanga amesema mafanikio makubwa yaliyopatikana yametokana pia na usimamizi wa Karibu wa viongozi wa Serikali katika ngazi zote za utekelezaji ambapo wamekuwa wakiwahamasisha wananchi kutumia vizuri fursa hiyo ili waweze kuinua kiwango chao cha maisha na kutokomeza umaskini kwa kasi kubwa zaidi.

Benki ya Dunia pamoja na taasisi nyingine za Kimataifa imekuwa ikichangia fedha kugharamia Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ambao kwa sasa unahudumia takribani kaya Milioni Moja na Laki Moja Tanzania Bara, Unguja na Pemba,Mpango ambao umekuwa chachu ya maendeleo kwa Kaya za Walengwa .Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr. Hafez Ghanem (watatu kulia) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na kuuzwa na Walengwa wa TASAF katika eneo la Mamboleo,Temeke kama njia mojawapo ya kujiongezea kipato.
Baadhi ya walengwa wa TASAF wa Mtaa wa Mamboleo-Temeke jijini DSM wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa WB kanda ya Afrika Dr. Hafez Ghanem na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga kulia kwa Makamu huyo wa Rais wa WB.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika, Dr. Hafez Ghanem akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi ambao wazazi wao wako katika Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na serikali kupitia TASAF.
Makamu Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika,Dr.Hafez Ghanem,akivishwa skafu alipowasili kwenye mtaa wa Mamboleo,wilayani Temeke jijini DSMalipokutana na Walengwa wa TASAF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...