MAJESHI ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yapo imara kupambana na vitendo vya uvunjifu wa amani katika nchi wanachama baada ya kuhitimisha mazoezi ya pamoja yaliyozikutanisha nchi hizo mkoani Tanga .

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ulinzi Dr Husein Mwinyi wakati wa kufunga mazoezi hayo ambayo yalikuwa na malengo ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi,uharamia,majanga na kujenga uchumi imara katika nchi wanachama.

Aidha Dkt Mwinyi alisema kumekuwepo na ufanisi wa hali ya juu wa utayari wa kukabiliana na majanga kama hayo hivyo jukumu lipo kwa vikosi hivyo kujiamini na kutumia mbinu walizopata ili kuzisaidia nchi zao. “Tunaimani sasa baada ya mazoezi haya kwanza vikosi vyetu vitakuwa imara zaidi lakini ni wakati wa kuanza kupambana na matukio kama hayo si kwa nchi mojamoja bali kwa kushirikiana zaidi”Alisema Dr Mwinyi.

Mazoezi hayo yalizikutanisha nchi zote wanachama ikiwa pamoja na Tanzania ambae ni mwenyeji,Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi huku Sudani kusini haikufika kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wao. Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi toka Nchini Kenya Balozi Rachael Omamo alisema mbali ya kubadilishana uzoefu katika Nyanja ya kiusalama bali mazoezi hayo yanajenga mahusiano bora kwa Nchi zote wanachama.

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi akizungumza wakati akifunga kufunga mazoezi ya ya mafunzo ya Ushirikiano Imara mwaka 2018 ya Kijeshi kwa vikosi vyanchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye eneo la Mlingano wilayani Muheza mkoani Tanga ambayo yalikuwa na malengo ya kukabiliana na vitendo vya kigaidi,uharamia,majanga na kujenga uchumi imara katika nchi 
Waziri wa Ulinzi wa Kenya Balozi Raychelle Omamo akitoa salamu kwenye ufungaji huo wa mafunzo 
Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo akizungumza katika halfa ya ufungaji wa Mafunzo hayo yaliyifanyika kwenye eneo la Mlingano wilayani Muheza Mkoani Tanga 
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi kushoto akiwa na Waziri wa Ulinzi wa Kenya Balozi Raychelle Omamo
Vikosi mbalimbali vikipita mbele ya mgeni rasmi leo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...