Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii.

KLABU ya Mbao FC inayoshiriki Ligi kuu Tanzania Bara imealikwa kwenye michuano ya Sports Pesa Super Cup inayotarajiwa kuanza Januari 22 mwaka 2019.

Ikiwa ni mara ya tatu ya michuano hiyo tangu ianzishwe hapa nchini ambayo inazikutanisha timu za Tanzania na Timu za Kenya zinazo dhaminiwa na Kampuni hiyo ya Kubashiri ( Sports Pesa)

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mkurugenzi Mtendaji wa Sports Pesa Tarimba Abas amesema kuwa sababu ya kuialika Mbao FC kwenye michuano hiyo ni kutokana na Klabu hiyo kuonesha ushindani mkubwa kwenye Ligi kuu Tanzania Bara.

Kwa upande wa uongozi wa Klabu ya Mbao FC kupitia kwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo Solly Zephania Njash amesema anaishukuru Kampuni ya Sports Pesa kwa kuialika timu hiyo kwaajili ya kushiriki michuano hiyo na wanaamini watafanya vizuri kwenye michuano hiyo.

"Naishukuru Sports Pesa kwa kutupa heshima hii ya kutualika katika michuano hiyo na mualiko huu kwetu sisi ni Challenge kubwa kwa sababu tutakutana na timu za kigeni ambazo hatujawahi kucheza nazo, hivyo ni jambo jema kwetu na nazikaribisha pia timu za Simba,Yanga na Singida katika michuano hii.Michuano hiyo itashirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya ambapo kwa Tanzania timu hizo ni Simba,Yanga,Singida United na Mbao FC kwa upande wa Kenya ni Gor Mahia,Kariobangi Sharks,Bandari FC na AFC Leopards.

Mshindi wa michuano hiyo atajishindia kitita cha Dola za Marekani 30000 na pia atacheza na timu ya Everton FC kutoka Uingereza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Sports Pesa Tarimba Abas akizungumzia michuano ya Sports Pesa Super Cup inayotarajiwa kuanza Januari 22 mwaka 2019.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...