Waziri wa Maji Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) amevunja mikataba miwili inayohusu kandarasi ya ujenzi wa miradi ya maji kwa kampuni mbili za kimataifa. 


Kampuni hizo ni Overseas Infrastructure Alliance (India) Pvt. Ltd yenye mkataba Na. ME-011/2011-2012/W/05 iliyokua inatekeleza Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Lindi mjini na kampuni ya Spencon Services Ltd yenye mkataba Na. ME-011/2011-2012/W/05 iliyokua inatekeleza Mradi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira wa Kigoma mjini. Mikataba hiyo imevunjwa kutokana na uzembe wa wakandarasi hao kuchelewa kukamilisha miradi.

Profesa Mbarawa amefafanua kuwa mikataba ya wakandarasi hao imevunjwa kutokana na kufilisika kifedha na kusababisha kukosa uwezo wa kumalizia kazi ndogo iliyokuwa imebaki na kukamilisha miradi hiyo, kulikopelekea wananchi wa maeneo hayo kutopata huduma ya majisafi na salama kwa muda mrefu kinyume na matarajio ya Serikali hivyo kuvunjwa kwa mikataba.

Amesema hatua hiyo inatokana na miradi hiyo kuchukua muda mrefu kukamilika pamoja na juhudi za viongozi wa juu wa Serikali, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Waziri mwenyewe kwa nyakati tofauti.

Mkandarasi wa mradi wa maji wa Lindi mjini kampuni ya Spencon Services Ltd ilipaaswa kukamilisha mradi toka Tarehe 17 Machi, 2015 kwa mujibu wa mkataba wa awali ikashindwa na kuongezewa muda hadi Tarehe 1 Desemba, 2015 lakini mpaka kufikia leo mradi huo haujakamilika. Naye mkandarasi wa mradi wa maji Kigoma mjini kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance (India) Pvt. Ltd ilipaswa kukamilisha Tarehe 17 Machi, 2015 kwa mujibu wa mkabata wa awali, na ikaongezewa muda hadi Tarehe 23 Desemba 2015. Mradi huo haujakamilika mpaka sasa ukiwa umefikia asilimia 87 ya utekelezaji.
Waziri wa Maji, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (Mb) akiwa na Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dodoma kuhusu kuvunja mikataba ya Wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Maji ya Mkoani Kigoma na Lindi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...