Na Francis Godwin,Iringa

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) imemfikisha mahakamani  Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Alex Kimbe kupitia chama cha demokrasia na maendeleo ( CHADEMA) makosa mawili ya jinai kuomba na kupokea rushwa .

Kaimu kamanda wa takukuru mkoa wa Iringa Mweli Kilimali akizungumza leo na vyombo vya habari ofisibni kwake alisema kuwa meya huyo alipokea kiasi cha shilingi milioni 2 kutoka kwa mteja wao .

Alisema kuwa tukio la kukamatwa meya huyo lilitokea Novemba 15 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika Hotel ya Gentle Hills mjini Iringa .Kuwa meya huyo ambae ni diwani wa kata ya Isakalilo aliokea pesa hizo kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007.

Alisema meya Kimbe alipokea fedha hizo za mtego wa rushwa akiwa kwenye gari yake aina ya nadia yenye rangi ya Marron ikiwa na namba za usajili T 456 CKD iliyokuwa imeegeshwa katika eneo la kuegesha magari kwenye hoteli hiyo .“ Maafisa wa takukuru waliweza kumfuatilia meya huyo kwa muda mrefu na hivyo kuweza kumkamata akiwa amekwisha pokea fedha hizo za mtego kutoka kwa mtoa taarifa wao.
Kimbe akiwashukuru waliofika Mahakamani leo.
 Meya Alex Kimbe akifikishwa Mahakamani na Maofisa wa TAKUKURU leo
Meya Alex Kimbe akiwa Mahakamani leo 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...