Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo amempongeza na kumtaka Mwanatasnia wa Filamu Bi. Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa kuwa Balozi mzuri wa Tasnia ya Filamu nchini mara baada ya kupata Tuzo ya heshima kutoka nchini Uganda. 
 Pongezi hizo amezitoa leo ofisini kwake Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam alipokutana na Muigizaji huyo kuzungumzia masuala mbalimbali ya Maendeleo ya Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini. 
Bi. Fissoo alimkumbusha Monalisa na Wadau wote wa Sekta ya Filamu na uigizaji umuhimu wa kuendelea kutoa taswira chanya katika jamii hatimaye kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii. 
“Wewe ni mfano wa kuigwa katika jamii kutokana na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, kuithamini na kuiheshimu kazi yako, niwakumbushe Wadau wote kujifunza yale mambo chanya kutoka kwako” Alisema Fissoo. 
Kwa upande wake Monalisa alimshukuru Katibu Mtendaji Bi. Fissoo kwa kuendelea kuwapa ushrikiano akiwepo yeye mwenyewe na Bodi kuwa sehemu ya kuhimiza na kusimamia Maendeleo ya Tasnia ya Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini. 
Monalisa alimuahidi kuendelea kushirikiana na Bodi hiyo katika kuendeleza na kutangaza sekta nzima ya Filamu kila apatapo fursa ndani na n je ya nchi. 
“Bodi ya Filamu imekuwa ni muhimili mkubwa katika kuiongoza Tasnia ya Filamu nchini hivyo nitahakikisha naendelea kushirikiana nayo bega kwa bega ili tuweze kuipa heshima Tasnia na nchi yetu kwa ujumla kupitia kazi bora tutakazo zizalisha” 
Alisema Monalisa. 
 Monalisa amepata Tuzo ya heshima kama Mwanamke wa Mfano na mwenye Ushawishi kwa Jamii kupitia kazi zake za Uigizaji ambapo Tuzo hiyo kutoka nchini Uganda atakabidhiwa Tarehe 1 Disemba 2018 jijini Kampala.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) Bi. Joyce Fissoo (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na nguli wa Filamu nchini mara baada ya kumaliza kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Tasnia hiyo na kupokea taarifa ya kupata Tuzo ya heshima Mwanatasnia Yvonne Cherrie (Monalisa) kutoka nchini Uganda. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Monalisa (Masafa Mwalimu), anayefuatani Bi. Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa na wa kwanza kulia ni Bi. Suzan Lewis ambae pia ni Mama mzazi wa Monalisa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...