Mshindi wa nyumba na sh milioni 20 wa Biko, Prisca Msuya wa Mbezi jijini Dar es Salaam, amelia kwa uchungu mbele ya waandishi wa habari wakati anakabidbiwa hundi ya ushindi wake wa fedha na nyumba kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) iliyopo Kigamboni, huku akishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, mama huyo ambaye ni mjasiriamali mdogo wa duka, alisema kitu kinachomliza ni kushinda nyumba na sh milioni 20 kutoka Biko, huku akitokea kwenye maisha duni ya kuishi kwenye chumba na sebule. 

“Siamini macho yangu kwamba kweli nimeshinda nyumba kutoka Biko, maana maisha yangu ya nyuma anayajua Mungu, ingawa tangu Biko inaanza nilikuwa namuomba Mungu ili niweze kushinda zawadi za juu ikiwamo sh milioni 10, jambo ambalo Mungu amenitimizia mara mia moja. “Kwakweli namshukuru sana Mungu kwa zawadi hii pamoja na kuwaombea Biko katika mtazamo wao wa kuleta utajiri kwa watu wake, hivyo Watanzania wote naomba tucheze Biko kwa sababu ndio michezo halali unaoweza kutoa mamilioni pamoja na nyumba,”Alisema. 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta, alisema mchezo wao umeanzishwa kwa lengo moja la kuwakwamua Watanzania, wakiwamo wadau wa kubahatisha, akisema kila mtu anapoibuka na ushindi anazunguukwa na watu wanaotumia ushindi huo kuboresha maisha yao kwa pamoja. “Leo hii tunamkabidhi dada Prisca fedha na nyumba, ila tunaamini wapo watoto wake, mume na ndugu ambao kwa namna moja ama nyingine watakuwa wamekwamuliwa na mchezo wetu wa Biko. 

Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta wa pili kutoka kulia akimkabidhi hundi ya sh milioni 20 na nyumba iliyopo Kigamboni mshindi wao Prisca Msuya wa katikati aliyeibuka kidedea kwenye droo kubwa iliyochezwa juzi Jumatano. Wengine ni Afisa Leseni wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Catherine Lamwai kushoto akifuatiwa na Kajala Masanja Balozi wa Biko pamoja na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Tuntufye Mwambusi. Picha na Mpigapicha Wetu.

Mkurugenzi Mkuu wa Biko, Charles Mgeta akimkabidhi hundi ya sh milioni 20 na nyumba iliyopo Kigamboni mshindi wao Prisca Msuya aliyeibuka kidedea kwenye droo kubwa iliyochezwa juzi Jumatano. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...