Watalaam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) ambao walikua wakitoa huduma za afya kwa njia ya mkoba katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi SOKOINE wamehitimisha huduma hiyo leo kwa kuwahudumia zaidi ya wagonjwa 1103 na kufanyia upasuaji wagonjwa 47.

Maeneo ambayo wataalam wa Muhimbili wamehudumia kwa kushirikiana na wataalam wa Hospitali ya Sokoine ni upasuaji, magonjwa ya kike na uzazi, meno, macho,watoto, magonjwa ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya dharura, Radiolojia pamoja na magonjwa ya ndani.

Mbali na kutoa huduma hizo lakini pia watalaam wa Muhimbili wamewajengea uwezo kiutendaji wataalam wa hospitali hiyo pamoja na kuleta mabadiliko ikiwemo kuelekezwa jinsi ya kanzisha idara na kuzisimamia ili kuleta ufanisi katika utoaji huduma.

Akizungumza katika kikao cha tathimini ya utoaji huduma, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija amesema kuanzishwa kwa idara mbalimbali kutaleta mabadiliko makubwa katika kutimiza majukumu yao kuanzia ngazi ya chini mpaka ya juu.Hivyo amewataka watumishi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi kukubali mabadiliko ili kufikia malengo ya utoaji huduma bora.

‘’Hospitali hii ni ya rufaa, wananchi wanaitegemea katika kupata huduma hivyo lazima tutoe huduma bora na zenye viwango vya juu na yote yatafanikiwa endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake’’.amesisitiza Dkt. Shija.Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu amemsihi kiongozi wa hospitali hiyo kutowaonea aibu watumishi wanaokwamisha maendeleo ya hospitali.
Ameto wito kwa watumishi hao kutumia fursa zinazojitokeza ili kupata ujuzi Zaidi.

Mara baada ya kumaliza kutoa huduma katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Lindi wataalam hao wataelekea Hospitali ya Ligula Mtwara kwa ajili ya kutoa huduma na kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo. 

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Sokoine Dkt. Jumanne Shija akizungumza katika kikao cha tahimini ya utendaji kilichohusisha wataalam wa MHN pamoja na wataalam wa hospitali hiyo. 
Baadhi ya wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na wataalam wa Hospitali ya Sokoine wakimsikiliza Kaimu Mganga Mfawidhi katika kikao hicho.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya kike na uzazi kutoka MNH Geofrey Marandu akielezea jambo katika kikao hicho. 
Katibu wa hospitali hiyo Boniface Lyimo akitoa neno la shukrani wakati wa kikao hicho. 
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na watalaam wa afya wa Idara ya Upasuaji mara baada ya kuanzishwa kwa idara hiyo kufuatia ushauri uliotolewa na wataalam wa MNH. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...