Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo  kikuu cha Dodoma ( UDOM)kitivo cha elimu amekwama nauli ya kufika chuoni  baada ya wazazi  wake kutamka bayana kuwa hawana uwezo hata  ya kupata nauli ya kumsafirisha  binti yao kufika chuoni .
Bahati  Njete (21) mkazi wa Minazini wilayani Namtumbo amechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma  huku  wazazi wake hawana  uwezo  hata wa kumpatia  nauli ya kufika  chuoni  ili  akaendelee  na masoma yake.
Akiongea  na Ofisa ustawi wa jamii wilaya ya Namtumbo Irene Kitula ofisini kwake  Bahati alisema  wazazi wake wanahali ngumu za kimaisha na mafanikio aliyoyapata ni kutokana na misaada ya wasamaria wema  ambao walijitolea kwa hali na mali kumsaidia toka kidato cha kwanza  hadi cha sita.
Aidha  Bahati alidai kumaliza elimu ya sekondari katika sekondari ya kata Narwi  iliyopo wilayani Namtumbo na kisha kuchaguliwa kuendelea na masomo kidato cha sita katika shule ya sekondari ya  Igowole  iliyopo mkoa wa Njombe.
Ofisa  ustawi wa jamii alimfikisha mwanafunzi huyo mpaka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Namtumbo ili apatiwe kibali cha kuomba kuchangiwa fedha  kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufika chuoni  na zimsaidie akiwa chuoni pia.
Kwa  mujibu wa  mwanafunzi mwenyewe Bahati  alidai kusoma katika mazingira magumu kulingana na hali ngumu za wazazi wake lakini anawashukuru  wasamaria wema walioweza kumchangia kwa hali na mali mpaka kufikia hapo alipofikia .
Hata hivyo anaendelea kuwaomba wasamaria wema hao wasichoke  kumsaidia  bali waendelee kumsaidia kupitia namba yake ya simu 0718792037 ili aweze  kutimiza ndoto zake  za maisha baada ya kumaliza chuo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...