NA LUSUNGU HELELA
Naibu Waziri Wizara ya  Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewatoa hofu watumishi wa Taasisi zenye jukumu la kulinda na kuhifadhi Wanyamapori na Misitu nchini kuwa hakuna maslahi yao yatakayobadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu

Naibu Waziri Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ikiwa ni mara yake ya kwanza  kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa  kushika wadhifa wa Naibu Waziri katika Wizara hiyo  nyeti kwa uchumi wa nchi. Amesema ziara yake imelenga kuzifahamu Taasisi  anazoziongoza ili kujua namna zinavyotenda kazi na  changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.

Akizungumza kuhusu utendaji wa Jeshi USU, Naibu Waziri Kanyasu amesema kufuatia mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka katika mfumo wa kiraia na kuwa Jeshi USU kutakuwa na mabadiliko kiutendaji yatakayoendana na taratibu za Jeshi USU lakini utakaoheshimu na kulinda maslahi ya watumishi.   Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa, uanzishwaji wa Jeshi hilo haukusudii kubadili maslahi ya watumishi hao  na endapo maslahi hayo yatabadilika basi yatakuwa na mabadiliko chanya kwao.

Naibu Waziri Kanyasu ameongeza kuwa Jeshi USU litaongeza nidhamu uwajibikaji na maadili kwa watumishi wa sekta ya Maliasili na  Utalii ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili na si vinginevyo. Katika hatua nyingine,  Naibu Waziri Kanyasu ameiagiza Menejimenti ya Mamlaka ya  Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ibuni  vivutio  vipya vya  Utalii vitakavyosaidia  kuongeza  mapato kwa Serikali kwa kuzingatia majukumu makuu ya Taasisi.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa pili kushoto) akimsikiliza  Mhifadhi ,kuu  wa Mamlaka ya Hifadhi ya enoe la n Ngorongoro, Dkt.Freddy Manongi  wakati  alipowatembelea jana katika  Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuzungumza na  kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi 
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto) akipewa maelezo na Dkt. Maurus Msuha (katikati) wakiwa kwenye sehemu ya kuonea wanyamapori (View point) ya Ngorongoro Kreta wakati alipotembelea jana  kwa ajili ya  kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi
 Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  wakati alipowatembelea jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu  akipewa maelezo na Juma Hamadi jinsi mfumo wa malipo unavyofanya kazi kwa watalii wanaoingia katika  Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro

                       (PICHA NA LUSUNGU HELELA-WMU) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...