Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameipongeza Serikali ya Uturuki kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania hususan katika kukuza biashara, uwekezaji na utalii.

Mhe. Dkt. Ndumbaro ametoa pongezi hizo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam tarehe 18 Novemba 2018 kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni 7 makubwa ya uwekezaji kutoka Uturuki.

Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema kuwa, ziara ya ujumbe huo nchini ambayo itafanyika kuanzia tarehe 18 hadi 24 Novemba 2018 ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Uturuki na wadau mbalimbali katika kutekeleza diplomasia ya uchumi ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kwenye kutafuta na kuleta wawekezaji wenye nia ili wawekeze katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi.

Akielezea ziara hiyo, Dkt. Ndumbaro alieleza kuwa, ujumbe wa wawekezaji kutoka Makampuni hayo ya Uturuki hapa nchini utatembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Simiyu. Alisisitiza kwamba ujumbe huo umechagua mikoa hiyo kwa malengo mahsusi ya kuwekeza katika sekta ya viwanda ikiwemo Kiwanda cha nguo, kiwanda cha sukari, kiwanda cha saruji, kiwanda cha vifaa vya ujenzi, kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa na uwekezaji kwenye sekta ya nishati kwa mkoa wa Simiyu. 

Aidha, kwa mkoa wa Dodoma ujumbe huo una nia ya kuwekeza katika ujenzi wa maduka makubwa (shopping malls), ujenzi wa majengo mbalimbali (real estate) na ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya kimataifa. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo) pichani kuhusu ziara ya ujumbe wa Makampuni 7 makubwa ya uwekezaji kutoka Uturuki itakayofanyika nchini kuanzia tarehe 18 hadi 24 Novemba, 2018. Ujumbe huo utatembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Simiyu kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya nguo, kiwanda cha kuongeza thamani bidhaa za kilimo, ujenzi wa maduka makubwa na hoteli za kimataifa. Mkutano huo na waandishi wa habari ulifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 18 Novemba, 2018. 
Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Davutoglu nae akizungumza wakati wa mkutano huo kuhusu ziara ya ujumbe kutoka Uturuki huku Mhe. Dkt. Ndumbaro akisikiliza
Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Ali Davutoglu (kushoto) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Jestas Nyamanga (katikati) pamoja na Afisa kutoka Ubalozi wa Uturuki wakifuatilia mkutano kati ya Dkt. Ndumbaro na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) 
Mkutano ukiendelea 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...