NA ELISA SHUNDA,KIBAHA
KONGAMANO la Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Iimetoka na Azimio la Pamoja la Wazazi katika Jamii Husika Kuhakikisha Inasimamia Maadili ya Vijana kwa Kuwa Chanzo cha Mmomonyoko wa Maadili Unaanzia kwenye vitongoji na mitaa ambako familia zao ndipo zinapoishi.

Maadili ni Mjumuisho wa Tabia Watu Zinazokubalika Mahali Fulani au Katika Jamii Fulani au Jumuiya Fulani au Nchi, Mjumuisho wa Tabia za Watu Unatokana na Kujumuisha Tabiaza Mtu mmoja Mmoja Tabia Hizi Ndizo Zinatufikisha Kule Tunapokuthamini.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kibaha Mjini,Edwin Shunda,alisema kuwa kwa mjumuisho wa kongamano hilo lililoshirikisha wadau mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali,wananchi na wanachama wa CCM imeazimia kwa pamoja kuwa mmomonyoko wa vijana katika maadili yao inatokana na malezi ya wazazi lakini pia katika mitaa na vitongoji ambavyo vijana hao wanatokea hakuna malezi ya pamoja ya wazazi kwa vijana wa sehemu husika kwa kuogopa lawama kwa wazazi wa motto au watoto waliovunja hayo maadili.

“Katika majadiliano yaliyofanyika leo katika kongamano hili la maadili wajumbe wengi na wadau mbalimbali wamesema sababu kubwa inayochangia kupolomoka kwa maadili kwa watoto wetu ni wazazi sisi kwa sisi wenyewe kuogopana kuwa huyu mtoto siyo wangu ukimuadhibu au kumkanya kwa kosa ulilomkuta nalo kwa hali ya sasa unaweza ukanunua ugomvi kwa familia ya mtoto aliyefanya kosa hivyo kupitia kongamano hili tumeazimia kwa pamoja tunapotoka hapa tunaanzisha mabaraza ya jamii yatakayoanzishwa kwenye vijiji na mitaa kwa ajili ya kusimamia malezi na maadili ya watoto wetu” Alisema Mwenyekiti Shunda.

Aliongeza kwa kusema maazimio hayo pia yameitaka jumuiya ya wazazi itoe maelekezo kwa mwenyekiti wa halmashauri na katibu wa baraza la madiwani ni wajumbe basi wapewe maagizo hayo ili kwa utaratibu ulio sahihi maazimio hayo yawasilishwe kwenye halmashauri ya wilaya na wao kwa utaratibu wa uanzishwaji wa sheria ndogo juu ya uanzishwaji na uendeshaji wa mabaraza hayo ya jamii.

“Kutokana na Tulichokijadili katika Kongamano pia mabaraza hayo yataanzisha na kutekeleza dhana ya uwajibikaji wa kijamii badala ya jamii kuilaumu serikali na vyombo vya dola jamii kwa pamoja itahakikisha inasimamia majumba ya starehe hayajengwi jirani na makazi ya watu ili kuwatenga watoto na majumba hayo,watoto chini ya umri wa miaka 18 hawaingii kabisa kwenye majumba ya starehe,udhibiti wa mabanda ya video mitaani katika kusimamia kwa usiri filamu zinazoonyeshwa zisiwe za kuvunja maadili kwa vijana hao ambapo athari yake ni kubwa sana;

“Udhibiti wa sherehe mbalimbali za kijamii zitakazokuwa na sura ya kuchochea mmomonyoko wa maadili kwa vijana pamoja na utoaji wa vibali vya kufanyia shughuli hiyo,pia jamii ndio itakayokuwa ikiongoza serikali katika mtaa na vijiji chake katika kushughulikia matatizo ya sehemu husika pindi yanapotokea siyo kuwaachia wenyeviti na wajumbe kushughulikia tatizo hilo badala yake kwa pamoja watashirikiana kulitatua changamoto iliyojitokeza” Alisema Mwenyekiti Shunda.

Pia Mwenyekiti huyo alisema kuwa maazimio waliyopewa katika kongamano hilo ni uongozi wa jumuiya ya wazazi ihakikishe kuwa ajenda ya mahudhurio ya wananchi kwenye mikutano mikuu ya mitaa na vijiji inasimamiwa kimkakati ili wahudhurie kwa wingi ili wapate kujadili kero zao na pia halmashauri ihakikishe wale watakaopata huduma za jamii mbalimbali kama vile mikopo ya vijana wawe ni wale walioanzisha ajenda hiyo kwa kuhudhuria kwenye mikutano ya mitaa na vijiji ambao watakaokuwa wameorodheshwa kwenye madaftari ya mitaa na vijiji na kutoa taarifa za maendeleo kwenye mikutano ya mitaa,Hii Itahusu vilevile uanzishwaji wa vyama vya ushirika vya aina mbalimbali vianzie kwenye mikutano ili iwe mvuto kwa vijana kuhudhuria kwenye mikutano ili kuwasaidia vijana hao kupokea ushauri kutoka kwa wazazi wao,kuchangia na kutoa mawazo yao kwa jamii husika inayowazunguka.

Mwenyekiti Shunda Alimaliza kwa Kusema kuwa Kongamano limeshauri kuwe na utaratibu makini wa ufuatiliaji wa karibu wa maadili ya watanzania inawezekana kurekebishika na wananchi wakaishi kwa heshima,wananchi wakiwezeshwa kwa kujengewa stadi za uwajibikaji wa kijamii wataweza kuendesha mambo yao wenyewe na kuyasimamia bila kuhitaji nguvu nyingi kutoka ndani au nje ya nchi,hii itapelekea kujenga wazalendo wa kweli wa nchi hii na wakasiamama kama taifa lenye uwezo wa kujenga nchi katika misingi ya ujamaa na kujitegemea kama ilivyo kwenye katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kibaha Mjini,Edwin Shunda (katikati) akizungumza katika Kongamano la Maadili lililokuwa likijadili mmomonyoko wa maadili ya vijana yaliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Elimu Kibaha jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo,Mwalimu Charles Maguye na Katibu wa Jumuiya Hiyo,Ruth Rutashiba. Picha na Elisa Shunda

 Wajumbe na wanachama wa Chama Hicho wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...