NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) ndugu Humphrey Polepole amesema njia pekee ya CCM kulipa wema kwa wananchi ni viongozi wake kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuleta maendeleo endelevu nchini. 

Amesema wananchi wamekiamini Chama na kukipa ridhaa ya kuongoza Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokana na usimamizi na utekelezaji mzuri wa Sera zake kwa jamii. Rai hiyo aliitoa leo (jana) katika hafla ya kukabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama kwa wananchi wa Jimbo la Tunguu huko katika ukumbi wa T.C uliopo Dunga Wilaya ya Kati Unguja. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mipira hiyo kwa uongozi wa Jimbo la Tunguu kwa niaba ya wananchi, Ndugu Polepole amesifu juhudi za kuwatumikia wananchi zinazofanywa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo hilo.Polepole aliwataja viongozi hao ambao ni Mbunge wa Jimbo hilo Khalifa Salum Said na Mwakilishi wa Jimbo hilo Simai Mohamed Said kuwa wametoa mipira hiyo kwa lengo la kumaliza changamoto ya ukosefu wa huduma za maji. 

Ndugu Polepole alisema Viongozi wa Chama na Serikali hasa Wabunge, Wawakilishi na Madiwani nchini wanatakiwa kuendeleza utamaduni wa kufanya kazi na kuwapelekea wananchi maendeleo na sio ahadi za uongo.Katibu huyo wa NEC,Polepole alifafanua kuwa maisha ya mwanadamu yeyote yanahitaji maji hivyo Kitendo cha kuwapelekea wananchi huduma hiyo ni kuharakisha maendeleo ya jimbo kwani wananchi watafanya shughuli za kujiingizia kipato kwa utulivu.

Kupitia hafla hiyo, kiongozi huyo aliwataka viongozi wa majimbo mengine Zanzibar kuiga mfano huo wa kutatua kero za wananchi ili ifikapo mwaka 2020 CCM iwe imetekeleza ahadi zote zilizotolewa katika Uchaguzi Mkuu wa Dola uliopita. Katika maelezo yake Polepole,alitangaza rasmi kuwa kiongozi yeyote atakayeshindwa kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 asitarajie kupewa tena nafasi ya uongozi kupitia Chama Cha Mapinduzi kwani anakuwa haitoshi kiutendaji. 
KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM mara baada ya kukabidhi miundombinu hiyo ya kusambazia maji safi na salama katika vijiji vya Jimbo la Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akimkabidhi mipira ya kusambazia maji safi na salama Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Nd. Simai Mohamed Said kwa niaba ya wananchi wa Jimbo hilo.
KATIBU wa NEC, Idara ya Itkadi na Uenezi CCM Humprey Polepole akifukia mipira ya maji safi na Salama katika Kijiji cha Bungi Jimbo la Tunguu.
BAADHI ya wanachama na viongozi wa CCM wakimsikiliza nasaha za Katibu huyo Polepole mara baada ya kukabidhi mipira ya kusambaza maji iliyonunuliwa na Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu kwa ajili ya kutatua kero za wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...