Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) linashiriki maonyesho ya viwanda vidogo vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara kuanzia Novemba 5 hadi 11,2018. Maonyesho hayo yalianzia mkoani Simiyu, na sasa yanaendelea mkoa wa Mtwara na yatamalizikia mkoani Tanga.

Maonesho haya yenye lengo kuu la kuwasidia wajasiriamali kupata masoko ya bidhaa zao, kujifunza kupitia wenzao na kujenga mahusiano baina ya taasisi moja na nyingine, yameshirikisha taasisi takribani 16 za kiserikali na zisizo za kiserikali pamoja wajasiriamali zaidi ya 278 kutoka mkoa wa mtwara na mikoa ya jirani.

NSSF kupitia maonesho hayo imepata fursa ya kuwafikia washiriki Mbalimbali na kutoa elimu kwa ukaribu zaidi juu ya huduma zitolewazo na shirika pamoja na hifadhi ya jamii kwa ujumla.Baada ya kupatiwa elimu wajasiriamali wanapata nafasi ya kusajiliwa na kuwa wanachama wa nssf ili nao waweze kunufaika na mafao yote yatolewayo na shirika hili ambayo ni pamoja na matibabu bure kwao na familia zao.

Meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara,Ndugu
Stanley Millanzi  ametoa wito kwa wakazi wa Mtwara, mikoa ya karibu na nchi nzima kwa ujumla kutembelea banda la NSSF katika maonesho hayo ili kupata elimu na kujiandikisha, hususan baada ya Mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2018, ambapo NSSF ilipewa jukumu la kuwaandikisha na kuwapa hifadhi ya jamii wananchi wote waliopo katika sekta binafsi na sekta isiyo rasmi ikiwemo wajasiriamali. 
 Afisa uhusiano wa NSSF Rehema Urembo akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya katika banda la NSSF kwenye maonesho ya viwanda vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara
 Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya akiwa sambamba na Mbunge wa Mtwara Vijijini Mh Hawa Ghasi wakimsikiliza  Afisa uhusiano wa NSSF Rehema Urembo alipokuwa akitoa ufafanuzi wa baadhi ya huduma zitolowezo na Shirika hilo,kwenye maonesho ya viwanda vidogo yanayoendelea mkoani Mtwara

Meneja NSSF na PSSSF  mkoa Mtwara,Ndugu Stanley Millanzi  pamoja na Zaida Mhava wakimsikiliza Naibu Waziri wa viwanda Mhandisi  Stella Manyanya (hayupo pichani) kwenye  Banda la NSSF,wakati wa maonesho ya SIDO yakiendelea mkoani Mtwara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...