Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MSHAMBULIAJI mpya wa Klabu ya Azam FC, Obrey Chirwa, leo asubuhi ameanza kufanya mazoezi kwa mara ya kwanza kwenye timu yake hiyo mpya.

Staa huyo wa zamani wa Yanga na FC Platinum, amejiunga na Azam FC akitokea Nagoon ya Misri kwa usajili huru baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na timu hiyo.

Chirwa amejumuika mazoezini kwa mara ya kwanza na wenzake, wakati timu hiyo ikianza rasmi kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) dhidi ya Ruvu Shooting utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Novemba 22 mwaka huu.

Kwa mara nyingine tena Cirwa anaungana na rafiki yake wa siku nyingi, Donald Ngoma, ambaye walicheza naye Platinum ya Zimbabwe kwa takribani miaka sita kabla ya kufanya tena kazi pamoja wakiwa Yanga na sasa Azam FC, mara zote mbili hapa Tanzania wakiunganishwa na Kocha Mkuu, Hans Van Der Pluijm, ambaye kwa sasa anaifundisha Azam FC.

Mazoezi hayo yaliyosimamiwa na Kocha Pluijm, yalikuwa ni makali lengo kuu ni kurudisha ufiti kwa wachezaji baada ya mapumziko ya takribani siku sita.

Aidha mazoezi hayo yalihudhuriwa na wachezaji wote ukiondoa sita waliojiunga na timu za Taifa, nahodha Agrey Moris, Abdallah Kheri, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mudathir Yahya, Yahya Zayd (wote Taifa Stars) huku Nickolas Wadada akiwa na Uganda ‘The Cranes’.

Nyota mwingine Tafadzwa Kutinyu, ambaye alikuwemo mazoezini leo anatarajia kujiunga na timu ya Taifa ya Zimbabwe muda keshokutwa Jumatano.

Wakati mechi za ligi zikielekea raundi ya 14, kikosi cha Azam FC hadi sasa kinashika usukani kikiwa na pointi 30 baada ya kushinda mechi tisa na sare tatu huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote na nyavu zikitikiswa mara mbili tu.
Mshambuliaji mpya wa Azam Fc Obrey Chirwa akiwa katika mazoezi ya pamoja na klabu yake mpya hiyo kujiandaa na ligi kuu Tanzania Bara (TPL)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...