NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA

JESHI la Polisi Wilaya ya Tabora linaendelea kumtafuta mtu aliyesambaza ujumbe wa uongo juu ya kutekwa wa wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi ChemChem uliosababisha taharuki kwa wananchi na kupelekea kuharibu mali za Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tabora (OCD) John Mfinanga wakati akitoa ufafanuzi kwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora kwenye kikao cha robo ya kwanza.Alisema ujumbe huo ulisababisha kuwepo na uvunjifu wa amani ambao ulitokana na baadhi ya raia kuanza kuwashambulia Polisi na mgari yao na kupelekea kupasuliwa vyoo.

Mfinanga alisema hadi leo ikiwa saa 30 zimeshapita hakuna mzazi aliyejitokeza kutoa taarifa juu ya kupotelewa na mtoto jambo linaonekana lilikuwa na uongo na lenye nia ya kuleta vurugu katika jamii.“Waheshimiwa Madiwani ni mzazi gani anaweza kukaa zaidi ya masaa 24 mtoto wake amepotea hatoi taarifa…tunamtafuta aliyesambaza meseji hiyo ili hatimaye tumfikishe anapostahili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria” alisema.

Aliwataka Madiwani kusaidia kuwaelimisha wapiga kura wao wanapotoa taarifa ziwe za kweli ili zisisababishe taharuki na fujo katika jambo.Katika hatua nyingine Kamanda huyo wa Wilaya ya Tabora alisema Jeshi la Akiba Mgambo lipo kisheria na liko kwa ajili ya kusaidia majeshi mbalimbali yanapokuwa na uhitaji katika kutekeleza majukumu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...