*Ashirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke,DAWASA kupanda miti pemebezoni mwa mto Kizinga.

*Mito zaidi ya 10,000 kupandwa Mto Mzinga, kampeni kuendelea hadi Mto Ruvu
 
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa amewaomba wananchi kutunza vyanzo vya maji ili viwe endelevu na kuacha kulima pembezoni mwa mito.

Ameyasema hayo leo wakati wa upandaji miti aina ya Mitomondo pembezoni mwa mto Kizinga akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Akizungumza na wananchi wa eneo la Mtoni Mashine ya maji, Profesa Mbarawa amesema wananchi wanatakiwa kulinda vyanzo vya maji ili wapate majisafi na salama kwa manufaa yaona vizazi vijavyo.
 
Amesema, amehakikisha wanaanza kampeni maalumu kwa ajili ya kulinda vyanzo vya maji, na wakivilinda vizazi vijavyo vitapata maji safi na salama na serikali watapoteza pesa nyingi iwapo wananchi wataharibu vyanzo hivyo.

Amesema Serikali inatumia pesa nyingi kujenva miundo mbinu ya maji na iwapo vyanzo vikiharibikiwa na basi haitaweza kufanya kazi ya kusambaza maji safi na salama.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa akipanda mti kwenye Chanzo cha Mto Kizinga ikiwa ni kampeni ya Upandaji miti pembenzoni mwa vyanzo vya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akiwa anapamba mtikwenye Chanzo cha Mto Kizinga ikiwa ni kampeni ya Upandaji miti pembenzoni mwa vyanzo vya maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam ( DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akipanda mti kwenye Chanzo cha Mto Kizinga ikiwa ni kampeni ya Upandaji miti pembenzoni mwa vyanzo vya maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...