Na Mwamvua Mwinyi, Pwani 
JESHI la polisi mkoani Pwani, limekamata luninga kumi flat screen zenye thamani ya sh. mil.18, ambazo ziliibiwa katika matukio mbalimbali ya uvunjaji, mkoani humo. 

Aidha linamshikilia mtu mmoja jina limehifadhiwa baada ya kukutwa akiwa na madumu kumi yenye ujazo wa lita 20 ya mafuta aina ya dizeli  ,aliyoiba katika mradi wa ujenzi wa reli ya standard gauge , Soga wilaya ya kipolisi Mlandizi. 

Akithibitisha kutokea kwa matukio hayo, kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa alisema, wanashikilia watu nane kwa tuhuma za kuhusika kwenye matukio hayo. 

Nyigesa alieleza katika msako huo wamekamata jenereta mbili kubwa zenye thamani ya milioni 6.5 ambazo ni aina ya Euro power EP. 6500E na boss BG -2500 .

Alifafanua, vitu vingine vilivyokamatwa ni deki mbili, vingamuzi viwili, speaker mbili, music system mbili, home fieta moja, rimoti sita, speaker twiter mbili, flash moja kapeti za chini ya sakafu mbili, stendi ya vyombo moja na extention moja. 

Hata hivyo kamanda huyo alisema , mtuhumiwa aliyekamatwa kijiji cha Mperamumbi akiwa amepakia mafuta kwenye pikipiki aina ya sanlg namba MC. 197 BJD kutoka mradi wa standard gauge wanamhoji na atafikishwa mahakamani. 

Katika tukio jingine wamekamata pikipiki saba na bangi kiroba kimoja kilichokuwa kinasafirishwa kwenda kuuzwa. 

Nyigesa alibainisha, katika tukio hilo mmiliki wa pikipiki yenye namba za usajili MC 951 BSA  anaombwa kujisalimisha mwenyewe kituo chochote cha polisi ndani ya siku tatu vinginevyo watamsaka popote ili kueleza kuhusu bangi hiyo. 
Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa akionyesha baadhi ya luninga flat screen zilizoibiwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo (picha na Mwamvua Mwinyi)

Kamanda wa polisi mkoani Pwani (ACP)  Wankyo Nyigesa akielezea msako endelevu unaendelea mkoa humo huku akieleza kauli mbiu yake ya Tindua Tindua hadi kieleweke. (picha na Mwamvua Mwinyi)

Mmoja wa watu walioibiwa luninga zao, mzee Lebul Mfinanga (wa kulia aliyebeba luninga) akiwa ametoka kutambua luninga yake makao makuu ya polisi Pwani . (picha na Mwamvua Mwinyi) 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...