RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesema misaada mbali mbali iliyotolewa na Chuo Kikuu ‘Houkeland University Hospital’, imekwenda sambamba na dhamira ya muda mrefu ya Serikali ya kutoa huduma bora za tiba ya akili kwa wananchi wake.

Dk. Shein amesema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar, alipozungumza na ujumbe wa Madaktari wanne kutoka chuo kikuu cha ‘Houkeland University Hospital’ cha nchini Norway, ukiongozwa na Katibu Mtendaji Eivind Hamsen. Alisema kwa nyakati tofauti Serikali kwa kushirikiana na washirika wa maendeleo imekuwa ikifanya kila juhudi kuhakikisha inaimarisha upatikanaji wa huduma za tiba ya akili katika Hospitali yake iliopo Kidongochekundu mjini hapa na kuondokana na dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa eneo hilo ni ‘jela’ ya wagonjwa hao.

“Serikali imekuwa ikifanya kila juhudi kuimarisha Hospita hiyo, ili ionekane ni kituo cha tiba ya akili, sio tena jela ya wendawazimu kama ilivyokuwa ikitambulika mara baada ya kuanzishwa kwake”, alisema. Alisema juhudi hizo ziliambatana na uanzishaji wa sera mpya na sheria za uendeshaji wa hospitali hiyo, zikilenga kuleta mageuzi makubwa katika suala la upatikanaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Alisema tayari kuna mafanikio makubwa yaliofikiwa, katika upatikanaji wa huduma za tiba ya akili, huku mkazo ukielekezwa kukiimarisha zaidi. Katika hatua nyengine Dk. Shein alisema Zanzibar imepata mafanikio makubwa katika sekta ya Afya, kwa kuiimarisha Hospitali kuu ya Mnazi mmoja, Hospitali za Wilaya pamoja na vituo vya Afya Unguja na Pemba, kwa kuvipatia vifaa vya kisasa na mafunzo kwa madaktari wake.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania. Mhe. Hamdi.M.H.Abuali, alipofika Ikulu Zanzibar, leo kwa mazungumzo na kujitambulisha.tarehe 16/11/2018.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi Mpya wa Palestine Nchini Tanzania Mhe. Hamdi M.H.Abuali, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo na kujitambulisha leo 16/11/2018, Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Chuo cha “Houkeland University Hospital” kulia Mr. Eivind Hamsen -CEO,akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo.tarehe.16/11/2018.(Picha na Ikulu) 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka Norway Chuo Kikuu cha “Houkeland University Hospital” kulia Wairi wa Afya Zanzibar Mhe. Hamad Rashid Mohammed,anayefuata ni CEO Eivind Hamsen na John Wigum Dahil, wakifuatilia mazungumzo hayo wakiwa nje ya ukumbi baada ya mazungumzo yao leo Ikulu Zanzibar.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...