Shirika la Save The Children limekutana na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga katika mafunzo ya siku moja kwa ajili ya kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Novemba 19,2018 katika ukumbi wa Good Shepherd mjini Kahama, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.

Akifungua mafunzo,Macha aliwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.Alisema katika wilaya ya Kahama,halmashauri za Msalala na Ushetu zinaongoza kwa mimba na ndoa za utotoni kutokana na mila na desturi kandamizi,umaskini,tamaa za mwili,mazingira pamoja na maendeleo ya teknolojia ambapo simu za mkononi zimekuwa zikiongeza tamaa kwa wanafunzi.

“Waandishi wa habari mna nafasi kubwa katika vita hii ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa mnawafikia watu wengi zaidi kupitia habari zenu,Lazima wadau wote tushirikiane kutokomeza changamoto hizi ili watoto wetu wawe salama”,alisema.Aidha Macha aliwataka wananchi kuzingatia utawala wa sheria na kwamba serikali itaendelea kuwachukulia sheria watu wote wanaoshiriki kuwafanyia ukatili watoto.
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na shirika la Save The Children kwa ajili ya kukutana na kupanga mikakati ya kutokomeza ndoa na mimba za utotoni. Kushoto ni Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima - Picha zote na Kadama Malunde na Marco Maduhu- Malunde1 blog.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akielezea lengo la shirika hilo kutoa mafunzo kwa waandishi yaliyolenga kukutana na wanahabari na kuwaeleza hali halisi ya mimba za utotoni katika mkoa wa Shinyanga ili waweze kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii.
Mratibu wa mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni wa shirika la Save The Children,Mary Zebron akielezea miradi inayotekelezwa na shirika hilo ambayo ni elimu,ulinzi wa mtoto na mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi zinazochangia mimba na ndoa za utotoni.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...