KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd na SOS Children’s Villages Tanzania wameingia  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi, lengo likiwa ni kuwapatia fursa  mbalimbali hasa kiteknolojia ili kuendana na malengo ya milenia yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.

Katika mkataba huo StarTimes itasaidia programu mbalimbali za SOS Children’s Village katika Mikoa zaidi ya saba ikiwemo Unguja, Pemba, Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Iringa na Mufindi na program hizo zitalenga hasa kwenye kupanua nafasi za kujifunza na kukuza uzoefu miongoni mwa Vijana wa SOS Children’s Village. 

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makubaliano hayo mwanasheria mkuu wa Star Media (T) Ltd Justine Ndege amesema  kuwa kwa vijana waliopo, kazi yao ya kwanza sio kuwa na uhuru. Kwao jambo la msingi kwanza ni kuishi tofauti ya maisha huru yenye heshima na maisha yenye misukosuko na mahangaiko ndicho wanacholenga kukabiliana nacho.

Ndege amesema kuwa, Ushirikiano baina ya kampuni Startimes na  SOS Village utapiga hatua katika kuwapeleka Vijana katika soko la ajira na kuwapatia namna au njia za kujitengenezea kesho yenye uimara na uhakika zaidi katika jamii zao.

Kwa upande wake  Mkurugenzi mkuu wa SOS Childre’s Village Dvid Mulongo amesema kuwa moja ya mambo ambao StarTimes itafanya ni kuwapatia nafasi vijana kutoka SOS Villages Tanzania bara na Zanzibar kujifunza kwa vitendo kazi mbalimbali zilizopo kwenye kampuni yao, ushauri, mafunzo ya kiufundi kuhusu namna ambavyo StarTimes inafanya kazi hasa katika Idara ya Masoko na kuhusu bidhaa zake ili kukuza uelewa wa kazi na ajira kwa Vijana.
Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kuingia makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo
 Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo(kushoto)  wakisaini  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za SOS Children’s Villages Tanzania jijini Dar es Salaam.
 Mwanasheria Mkuu Star Media (T) Ltd, Justine Ndege(kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa SOS Children's Village, David Mulongo(kushoto)  wakipeana mikono mara baada ya kumaliza kuingia  makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kusaidia familia na watoto/Vijana wanaoishi katika changamoto ya mazingira hatarishi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za SOS Children’s Villages Tanzania jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja  

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...